Benki ya NMB imedhibitisha
uongozi na sifa yake ya kuwa taasisi kinara wa huduma za kifedha nchini
na isiyo kuwa na mpinzani, katika kulihudumia taifa baada ya kutwaa tuzo
18 za ubora za kitaifa na kimataifa.
Benki hiyo imetangaza
kuwa, tuzo 10 za kimataifa imwetunukiwa hivi karibuni kwa kuwahudumia
vyema wateja wake na watanzania wote kwa ujumla, pamoja na kuwa kinara
wa ujumuishaji wa kifedha nchini. Nne kati ya tuzo hizo, zimetolewa kwa
Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Bi. Ruth Zaipuna kwa kuwa kiongozi
bora.
Akizungumza katika hafla ya kuzitangaza tuzo hizo, Bi,
Ruth alizitaja baadhi ya tuzo hizo kutoka kwenye majarida ya kimataifa
zikiwa ni pamoja na:
· Benki Bora Tanzania kwa mwaka 2022 - Kutoka Jarida la Global Brands Magazine
·
Benki Bora ya Wateja Binafsi na Biashara – Kutoka Jarida la World
Economic Magazine, Jarida la International Business Magazine na Jarida
la Global Banking and Finance Review
· Benki Bora katika Kilimo Biashara - Kutoka Jarida la Global Brands Magazine
· Ubunifu Bora katika Huduma za Kibenki kwa Wateja Binafsi Tanzania - Kutoka International Bankers Award
· Benki Bora kwa Wateja Maalum – kutoka International Bankers
·
Afisa Mtendaji Mkuu Bora kwa Mabenki nchini Tanzania – kutoka Jarida la
World Economic Magazine, Jarida la Global Brands Magazine na African
Bank 4.0 Summit
· Hatifungani Bora ya Mwaka 2022 - kutoka
Mtandao wa Mitaji kwa Wajasiliamali Wadogo na wa Kati ambao
wameshirikiana na nchi za G20 na IFC.
Tuzo hizi kutoka majarida
na taasisi zinazoheshimika duniani, zimeitambulisha Benki ya NMB kitaifa
na kimataifa, hivyo basi, kuitambulisha sekta na nchi yetu kimataifa.
Lakini pia, zinadhihirisha imani kubwa na heshima waliyonayo sokoni.
Kwa
upande wa tuzo za kitaifa, NMB ilishinda tuzo tatu za Mamlaka ya Mapato
(TRA) ikiwemo ile ya Mshindi wa Jumla ya taasisi zinazolipa kodi kubwa
na kwa kuzingatia misingi na kanuni bora za ulipaji kodi.
Akizungumza
kabla ya kupokea tuzo hizo, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya NMB, Bw.
Benson Mahenya, alisema benki hiyo ina kila sababu ya kujivunia tuzo
hizo, kwani ni matokeo ya kazi kubwa inayofanywa na manejimenti pamoja
na wafanyakazi wote kwa ujumla. Aliongeza kua, mafanikio hayo yametokana
na ubora na viwango vya kimataifa vya huduma zote zinazotolewa na Benki
ya NMB pamoja na uendeshaji wake. Baadhi ya Tuzo kati ya 18 za kitaifa na kimataifa ilizotunukiwa Benki ya NMB.
Wajumbe
wa Bodi ya Wakurugenzi NMB wakiwa na Menejimenti ya NMB, katika picha
ya pamoja wakiwa na baadhi ya tuzo ilizoshinda benki hiyo, baada ya
kuzitangaza kwenye hafla iliyofanyika Makao Makuu ya NMB.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB,Bi. Ruth Zaipuna, akimkabidhi
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya NMB, Bw.Benson Mahenya moja ya
tuzo 18 za kitaifa na kimataifa katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya
benki hiyo jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia kushoto ni Mjumbe wa
Bodi ya NMB, Bw. Ramadhan Mwikalu na kulia ni Afisa Mkuu Wateja Binafsi
na Biashara wa Benki ya NMB, Bw.Filbert Mponzi.
Thursday, November 24, 2022

Home
HABARI
BENKI YA NMB YATWAA TUZO 18 BAADA YA KUTHIBISHWA TAASISI KINARA WA HUDUMA ZA KIFEDHA NCHINI
BENKI YA NMB YATWAA TUZO 18 BAADA YA KUTHIBISHWA TAASISI KINARA WA HUDUMA ZA KIFEDHA NCHINI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment