HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 23, 2022

Airtel Money yazindua AFRICA Bila Mipaka, tuma na kupokea fedha nchi zote za SADC

 
· Kuendeleza suluhisho la huduma za kifedha wateja nchini kwa njia ya mtandao.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imetangaza kuzindua kampeni mpya kupitia huduma zake za Airtel Money itakayojulikana kama AFRICA Bila Mipaka, ambapo kwa sasa wateja wa Airtel Money wataweza kutuma na kupokea fedha papo hapo kwa nchi za jumuia ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC)

Nchi hizo za SADC ambazo mteja wa Airtel Money ataweza kutuma na kupokea fedha ni Malawi, Zambia, Zimbabwe Madagascar, Botwana, Lesotho na Namibia. Kwa uzinduzi huu Airtel imekamilisha kutoa suluhisho la huduma za Airtel money kutuma na kupokea fedha kwa nchi zote za Afrika.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza kampeni hiyo ya AFRICA Bila Mipaka Mkurugenzi wa huduma za Airtel Money Tanzania Isack Nchuda alisema, "Airtel siku zote tumekuwa tukija na huduma bunifu na ambazo zinagusa maisha ya kila siku ya wateja wetu ili kupanua zaidi Huduma ya Airtel Money.

Huduma hii tunayozindua leo inawaunganisha wateja wetu wanaotumia simu kufanya Miamala duniani na kuwezesha kufanikisha ndoto zao. Mteja ataweza Kupokea Pesa Papo hapo kwenye akaunti yake ya Airtel Money kutoka kwa ndugu au marafiki kutoka nchi za SADC, pia ikiwemo DRC na Sudan Kusini.


Huduma hii ni Salama na ya Uhakika na itapanua upatikanaji wa Huduma ya Kupokea/Kutuma pesa kwa wateja wetu katika maeneo ya mijini na vijijini kwani sasa wanaweza kupokea fedha moja kwa moja kwenye akaunti zao za Airtel Money bila ya kuwa na akaunti ya benki au huduma ya intaneti.

Dhamira yetu sisi Airtel ni kutoa huduma za kipekee, rahisi na nafuu kwa wateja wetu. Uzinduzi wa AFRICA Bila Mpaka na Airtel Money ni ushahidi mwingine kwetu kwamba tumedhamiria kukuza na kuwa suluhisho la kutoa huduma bora ya fedha kwa mtandao hapa nchini pamoja na kuweka usawa kwa jamii ya mjini na vijinini.

Tunaendelea kurahisisha kutuma pesa moja kwa moja kwenye akaunti za Airtel Money hapa nchini Tanzania kutoka nchi za SADC. Wateja wanaweza kupakua applikesheni au kutengeneza akaunti ili kuanza kutumia huduma hii na kuanza kutuma au kupokea fedha kwa familia na marafiki.

Huduma za kifedha kwa njia ya mtandao zimewaza kusaidia kupunguza gharama za kutuma au kupokea fedha, kuongeza unafuu pamoja na kurahishisha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa mtu binafsi au hata biashara. Kwa mtu anayepokea fedha kutoka nje ya nchi kwa sasa haitaji tena kusafiri umbali mrefu kwenye matawi ya benki ili aweza kupata fedha zake.

Airtel Money Tanzania kwa sasa imeunganishwa na makampuni zaidi ya 1000 pamoja na watoa huduma mbali mbali, vile vile Airtel Money imeunganisha zaidi ya taasisi 40 za kifedha. Airtel Tanzania inazidi kupanua huduma zake kote nchini kwa kasi kwani mpaka sasa tunayo maduka ya Airtel Money branches zaidi ya 3500 yanayotoa huduma mbalimbali pamoja na kuuza bidhaa zote za Airtel.


Mkurugenzi wa Huduma za Airtel Money Isack Nchunda (kati kati), Meneja Uhusiano Jackson Mmbando (kushoto) Airtel Tanzania na Meneja Huduma za Airtel Money Hellen Lyimo wakionesha bango baada ya kuzindua kampeni mpya kupitia huduma zake za Airtel Money itakayojulikana kama AFRICA Bila Mpika, ambapo kwa sasa wateja wa Airtel Money wataweza kutuma na kupokea fedha papo hapo kwa nchi za jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC).






Mkurugenzi wa huduma za Airtel Money Isack Nchunda (kati kati) akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam baada ya kuzindua kampeni mpya kupitia huduma zake za Airtel Money itakayojulikana kama AFRICA Bila Mpika, ambapo kwa sasa wateja wa Airtel Money wataweza kutuma na kupokea fedha papo hapo kwa nchi za jumuia ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC). Kushoto Meneja Uhusiano Airtel Tanzania na Meneja Huduma za Airtel Money (kulia) Hellen Lyimo.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad