NSSF YAENDELEA KUTOA HUDUMA KATIKA MAONYESHO YA TEKNOLOJIA YA MADINI GEITA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, October 1, 2022

NSSF YAENDELEA KUTOA HUDUMA KATIKA MAONYESHO YA TEKNOLOJIA YA MADINI GEITA


Waziri wa Madini, Mhe. Dotto Biteko leo tarehe 1 Oktoba, 2022 ametembelea banda la NSSF katika Maonesho ya Tano ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika katika viwanja vya uwekezaji (EPZA)Bombambili Mkoani Geita.
 
Ambapo aliupongeza Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) unavyohakikisha unatekeleza mpango wake wa kuyafikia makundi mbalimbali wakiwemo wachimbaji wadogowadogo wa madini katika maeneo mbalimbali.


Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF,Lulu Mengele akitoa maelezo kwa Waziri wa Madini, Mhe.Dotto Biteko leo 1 Oktoba, 2022 wakati alipotembelea banda la NSSF kwenye Maonesho ya Tano ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika katika viwanja vya uwekezaji (EPZA)Bombambili Mkoani Geita.

NSSF inashiriki Maonesho hayo kwa lengo la kutoa huduma mbalimbali za Hifadhi ya Jamii kwa wanachama na wananchi ikiwa pamoja na kusajili wanachama wapya wanaofika katika Banda la NSSF.
 
 


 


 

 

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad