WASIMAMIZI VYAMA VYA USHIRIKA KANDA YA KASKAZINI WAPATIWA MAFUNZO MFUMO MPYA WA KIELETRONIKI KUTUNZA NYARAKA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 12, 2022

WASIMAMIZI VYAMA VYA USHIRIKA KANDA YA KASKAZINI WAPATIWA MAFUNZO MFUMO MPYA WA KIELETRONIKI KUTUNZA NYARAKA


Na Mwandishi Wetu,Kilimanjaro

WASIMAMIZI wa vyama vya Ushirika Kanda ya kaskazini wamepatiwa mafunzo ya mfumo mpya wa kieletrokini utakaosaidia kutunza nyaraka na kumbukumbu za kifedha na mali za ushirika nchini.

Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo ya siku tatu katika Chuo Kikuu cha Ushirika kwenye ukumbi wa Pius Msekwa Mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, Katibu Tawala mkoa huo William Machum amesema uhifadhi duni wa nyaraka na kumbukumbu za vyama kwa baadhi ya vyama kupata hati chafu za ukaguzi .

"Uwazi na uwajibikaji katika kutunza taarifa za fedha na kutokuwepo na mfumo thabithi wa ufuatiliaji wa ukaguzi na usimamizi wa vyama ushirika nchini huchangia kwa kiasi kubwa vyama hivyo kuapta hati chafu na vingine kufa,"amesema.

Amesema kuwa mfumo huo utasaidia kuboresha kasi ya ukuaji wa vyama vya ushirika na kudhibiti ubadhilifu wa mali za ushirika.

Ameongeza Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi ya uanzishwaji na uendelezaji wa vyama vya ushirika ili kuhakikisha vyama vinakidhi matakwa na matarajio ya wanachama na kuchangia maendeleo ya Taifa.

Kwa upande wake Mhasibu Mkuu kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Valency Karunde amesema mafunzo hayo yamelenga kuwajenga uwezo maafisa ushirika kutoka kanda ya kaskazini pamoja warajis wasaidizi wa vyama vya ushirika wa mikoa hiyo.

Amefafanua kwamba mafunzo hayo pia ni pamoja usajili wa vyama ushirika kwa njia za kieletrokini ,na kwamba mafunzo hayo yatafanyika kwa siku tatu.

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad