TAFITI ZINAZOFANYWA NA WANATAALUMA ZITATUE MATATIZO YA KIMATAIFA- DKT. NDUMBARO - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 5, 2022

TAFITI ZINAZOFANYWA NA WANATAALUMA ZITATUE MATATIZO YA KIMATAIFA- DKT. NDUMBARO

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza wakati wa kufungua Mdahalo wa Wanataaluma wa Ndaki ya Sayansi za Jamii katika chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo Oktoba 5, 2022.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (UDSM), Profesa William Anangisye akizungumza wakati wa mdahalo wa wanataaluma wa Ndaki ya Sayansi za Jamii ikiwa ni Maandimisho ya Wiki ya Sayansi za Jamii pamoja na miaka 60 ya chuo Kikuu cha Dar es Salaam na miaka 57 ya ndaki ya Sayansi za Jamii.
Rasi wa Ndaki ya Sayansi za Jamii, Chuo Kikuu cha Dar es Salaama, Profesa Christine Noe Pallangyo akizungumza jijini Dar es Salaam leo Oktoba 5, 2022  wakati wa maandhimisho ya miaka 60 ya chuo Kikuu cha Dar es Salaam.Baadhi ya wanataaluma wa Ndaki ya Sayansi ya Jamii wakiwa katika maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo Kikuu cha Dar e Salaam leo Oktoba 5, 2022.

Picha za Pamoja.

Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro amewaasa wanataaluma na watafiti wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kufanya tafiti zenye kutatua matatizo katika jamii ya Tanzania na Kimataifa.

Hayo ameyasema leo Oktoba 5, 2022 wakati akifungua mdahalo wa wanataaluma na wanachuo wa ndaki ya Sayansi za Jamii Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, amesema kuwa nchi yetu haiishi kipekee inaishi katika Mazingira ya Kimataifa na mambo mengi yanayofanyika na wanataaluma yanakuwa na matokeo katika Mataifa Mengine na mambo wanayofanya mataifa mengine yanakuwa na matokeo nchi yetu.

"Nivizuri tunapofanya tafiti zetu zipande katika ngazi ya juu ya kujadili masuala ya kimataifa namna gani mambo yanayotokea nje ya nchi yetu kama vile taasisi za kimataifa mfano IMF na World Bank zinavyoshawishi utekelezaji wa mambo hapa nchini."Amesema Dkt. Ndumbaro

Amesema kuwa tafiti zifanywe kwa kuzingatia mambo ya ndani na mambo ya nje ya nchi ili matokeo yanapotekelezwa yasizingatie mambo ya ndani tuu ili tusikwame tunapotafuta msaada kutoka nje ya nchi.

"Tukizingatia mambo ya nje pamoja katika tafiti zetu yatatusaidia sana katika suluhisho ambalo ni halisia kabisa katika kutekeleza matatizo katika nchi."

Licha ya hayo Dkt. Ndumbaro ametoa wito kwa vyuo vingine wajitahidi kuzingatia viwango vya kimataifa katika kuzalisha wa nataaluma na kufanya tafiti na kutoa matokeo yanayolingana na viwango vya kimataifa.

Amesema kuwa wakizingatia viwango vya kimataifa itasaidia vyuo kutambuliwa kwenye kupanga vyuo vya kimataifa kwa kufikia viwango vya juu na kuvutia watu wengi kusoma nje ya nchi kuja kusoma nchini.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (UDSM), Profesa William Anangisye amesema ikumbukwe kwamba Chuo Kikuu cha Dar es Saalam Kilianzishwa kikiwa na wanachuo 14 na Kuwa na Mwanafunzi Mmoja wa Kike.

Kadri siku zinavyokwenda wamekuwa na uwekezaji wa hali ya juu na kuhakikisha kwamba idadi ya wanawake inaongezeka katika chuo kikuu cha Dar es Salaam. “Idadi kubwa ya wanafunzi imeongezeka kwa Upande wa wanawake na wanaume kwa asilimia 50 kwa 50.

"Hii ni kiu ya Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ni kuona kwamba idadi ya Wanawake na Idadi ya Wanaume inakuwa sawa katika suala zima la Taaluma na ngazi ya Uongozi wa juu." Amesema Prof. Anangisye

Amesema katika miaka 60 ya Chuo hicho wanachangamoto ya Sayansi kwani idadi ya Wanawake ipo chini ndio maana UDSM imeanzisha ufadhiri wa wanafunzi 50 kwa kila mwaka ambao wanasoma Masomo ya Sayansi, kwa kila Mwaka asilimia 25 tuu ndio wanawake wanaojiunga na masomo ya Sayansi katika chuo hicho na wanaufaulu mzuri katika masomo yao.

Amesema chuo Kikuu cha Dar es Salaam wamekuwa wanajitahidi kutoa fursa kwa wanataaluma wa kike katika nafasi za Uongozi. Pia amesema chuo hicho kinajivunia kuwa na viongozi wengi katika ngazi ya maamuzi ya nchi.

“Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimetoa Mchango Mkubwa katika Maendeleo ya Taifa hili katika kuisaidia serikali Mfano Mkubwa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho kikwete na wanachuo hicho wengi wamehusishwa katika katika nchi."

Katika miaka 60 ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam amesema wameongeza bajeti katika tafiti zinazofanywa na wanataaluma wa chuo hicho. “Sisi tumeona umuhimu wa Tafiti, tumewekeza kiwango kikubwa cha fedha ili kuwawezesha wanataaluma wanaofanya tafiti ili waweze kufanya tafiti ya maswali ya matatizo yanayoikumba jamii.

Kwa Upande wa Rasi wa Ndaki ya Sayansi za Jamii, Chuo Kikuu cha Dar es Salaama, Profesa Christine Noe Pallangyo amesema jamii na wataalamu wanamajukumu tofauti hivyo wanataaluma wanamajukumu ya kuibua sauti za jamii zilizojificha na kuziweka katika ngazi za kimataifa ili ziweze kujadiliwa.

Ndaki ya Sayansi za Jamii ilianza kuadhimisha miaka 60 ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Miaka 57 ya ndaki hiyo tangu kuanzishwa kwake, Septemba 29, 2022 kwa kufanya mahojiano mbalimbali pamoja na Kutembelea waraibu wa Dawa za kulevya wakiwa na kauli mbiu ya "Miaka 60 ya Umahiri wa Sayansi za Jamii Katika Taaluma, Tafiti naHuduma za kijamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad