HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, October 22, 2022

MATI SUPER BRANDS YATOA FIMBO NYEUPE 500 KWA WASIOONA

 


Na Mwandishi wetu, Babati
KAMPUNI ya Mati Super Brands Ltd, katika kuadhimisha siku ya fimbo nyeupe duniani, ambayo kitaifa imefanyika Mjini Babati Mkoani Manyara, imewakabidhi watu wasioona fimbo 500 za kutembelea.

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Mati Super Brands Ltd David Mulokozi amekabidhi fimbo hizo leo Oktoba 21 kwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, kazi, vijana, ajira na watu wenye ulemavu, Patrobas Katambi kwenye maadhimisho ya siku ya fimbo nyeupe duniani.

Mulokozi amesema Mati wametoa fimbo hizo nyeupe 500 kwa watu wenye ulemavu wa macho nchini ili kuunga mkono juhudi za serikali katika kuhudumia jamii.

"Mati tumeshiriki tangu kwenye makongamano tukiwa wadhamini hadi kwenye maadhimisho ya leo hivyo ili ndugu zetu wasioona wasiondoke mikono mitupu tumetoa fimbo hizo 500 Kwa," ameweza Mulokozi.

Amesema fimbo hizo za teklonojia rahisi ambapo zinajikunjwa na kukunjua na usiku zinakuwa na mwanga ili wakipita barabarani wenye vyombo vya moto wawaone kwa urahisi.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, kazi, vijana, ajira na watuwenye ulemavu, Patrobas Katambi, ambaye amemwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Mati wamefanya jambo kubwa kwani ni ibada kwa Mungu.

"Nakiri kupokea fimbo nyeupe 500 ambazo nazikabidhi kwa Mwenyekiti wa shirikisho la walemavu ambaye atajua namna ya kuzigawa kwenye mikoa yake," amesema Katambi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad