Kampuni ya simu ya Halotel na wafanyakazi wake leo wameshiriki katika
zoezi la kuchangia damu ikiwa ni sehemu ya kusheherekea na kuadhimisha
miaka 7 ya kampuni na utoaji wa huduma za mawasiliano.
Zoezi la
kuchangia damu ni majawapo ya taratibu ambazo Kampuni hiyo imejiwekea
kama msaada wa kurudisha shukrani kwa jamii pamoja na kuunga mkono
jitihada za serikali kupitia Sekta ya Afya katika kukabiliana na
changamoto ya uhaba wa damu katika hospitali au vituo vya kutolea huduma
za afya.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo katika ofisi za makao
makuu ya Halotel, Mkuu wa kitengo cha Bidhaa na Mawasiliano Halotel, Bi.
Sakina Makabu amesema kuwa katika kuhakikisha tunasaidia sekta hii ya
afya nchini, tumeona ni vyema kuchangia damu ili kuokoa maisha ya
watanzania wenye uhitaji hasa wa damu kwenye hospitali mbalimbali
nchini.
“Takwimu kupitia wizara ya afya nchini zinaonesha kwamba,
uhitaji wa damu ni mkubwa sana kwa kuwa damu inahitajika sana na mama
wajawazito, watoto, watu waliopata ajali pamoja na wanaofanyiwa
upasuaji", hivyo sisi kama Halotel kwa kushirikiana na Taasisi ya Tiba
ya Mifupa Muhimbili (MOI) tumeendeleza zoezi hili la kushiriki na
kuchangia damu kama hitaji maalum na ishara ya upendo kwa vitendo kwa
watanzania ambao pia ndio wateja wetu”. Alisema Sakina.
“Tunatambua
changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta ya afya hasa katika upande wa
uhitaji na upatikanaji wa damu katika hospitali na vituo vya afya kwa
wagonjwa na kuamua kuendelea kuunga mkono juhudi za utatuzi wa
changamoto hii kwa kujali na kutambua umuhimu kama kampuni na
wafanyakazi tumeamua kurudisha upendo huu kwa jamii. Aliongeza Sakina”
Akiongea
wakati wa zoezi hilo la uchangiaji damu mmoja kati ya wafanyakazi
waliochangia damu Bw;Dalili Musa alisema, “Tunajisikia furaha sana
kushiriki katika zoezi hili moja kwa moja kwasababu huduma hii
tuliyoifanya hapa kinaweza kuonekana ni kidogo ila kinaenda kuokoa
maisha ya watu na hakika ni kitendo cha kuonesha upendo na kinaleta
faraja Sana.
Kwa upande wa Uongozi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa,
Daktari wa dawa za usingizi katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili
(MOI), Bw; Juma Said Kabelele alisema “ Tumefarijika sana kwa kuja hapa
na kufanya zoezi hili la kutoa damu na kampuni ya Mawasiliano ya Halotel
na wafanyakazi wake, tunawashukuru sana kwa kuthamini afya za wananchi
lakini pia kwa kuunga mkono jitihada za kuisaidia sekta ya afya nchini.
Hii ni hatua kubwa na endelevu kwetu sisi katika kuimarisha ushirikiano
wetu na Halotel kwa kiwango cha juu hasa katika kuboresha sekta ya afya
kwa ujumla”.
“Tunapenda kutoa rai kwa watu binafsi, makampuni na
Taasisi mbalimbali kuweza kujitoa na kushiriki zaidi katika zoezi la
uchangiaji damu popote walipo nchini ili kuendelea kuipa ushirikiano
sekta ya afya nchini katika kukabiliana na tatizo la upungufu wa damu
katika benki ya taifa ya damu na hospitali mbalimbali maan mahitaji ni
makubwa sana na kila iku kuna idai kubwa ya wagonjwa wanaohitaji huduma
ya kuongezewa damu kulingana na tatizo husika la afya, hivyo utaweza
kuokoa Maisha ya watanzania wengi kwa Pamoja.” Aliongeza Mvungi.
Licha
ya kampuni ya simu ya Halotel kupiga hatua kubwa katika kusambaza
huduma za mawasiliano na intaneti yenye kasi na ubora wa hali ya juu ya
4G maeneo mengi nchini, kampuni hii imekuwa ikijihusisha na kutoa
misaada mbalimbali kwa jamii ya watanzania. Hii ni katika kuonesha jinsi
inavyothamini na kujali jamii ya watanzania kwa nyanja mbalimbali,
ikiwemo kuboresha sekta ya afya na zinginezo kama moja ya kipaumbele cha
kampuni ya hii kwa maendeleo ya watanzania na nchi kwa ujumla.Meneja
wa huduma za Kidigitali Halotel Caroline Majaliwa akishiriki katika
zoezi la uchangiaji damu lililoendeshwa na Kampuni ya simu ya Halotel
pamoja na Wafanyakazi kwa kushirikiana na Taasisi ya Tiba ya Mifupa
Muhimbili (MOI) ikiwa ni moja ya msaada wa kurudisha shukrani kwa jamii
katika kuelekea kilele cha kuadhimisha na kusherehekea miaka saba (07)
ya kutoa Huduma za mawasiliano hapana nchini pamoja na kuunga mkono
jitihada za serikali kupitia Sekta ya Afya katika kukabiliana na
changamoto ya uhaba wa damu katika hospitali au vituo vya kutolea huduma
za afya.
Baadhi
ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu ya Halotel Bw: Dalili Musa Mkuu wa
kitengo cha Usimamizi wa Mawasiliano ya Simu (wa kwanza Kushoto) na Bw;
Pius Joseph Tibasiga Afisa Manunuzi Halotel ( Wa pili kushoto)
wakishiriki katika zoezi la uchangiaji damu lililoendeshwa na Kampuni ya
simu ya Halotel pamoja na Wafanyakazi kwa kushirikiana na Taasisi ya
Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) ikiwa ni moja ya msaada wa kurudisha
shukrani kwa jamii katika kuelekea kilele cha kuadhimisha na
kusherehekea miaka saba (07) ya kutoa Huduma za mawasiliano hapana
nchini pamoja na kuunga mkono jitihada za serikali kupitia Sekta ya Afya
katika kukabiliana na changamoto ya uhaba wa damu katika hospitali au
vituo vya kutolea huduma za afya.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma na Mawasiliano Halotel Sakina Makabu
akiongea na waandishi wa Habari leo katika Ofisi za makao Makuu Halotel
wakati wa zoezi la uchangiaji damu lililoendeshwa na Kampuni ya simu ya
Halotel pamoja na Wafanyakazi kwa kushirikiana na Taasisi ya Tiba ya
Mifupa Muhimbili (MOI) ikiwa ni moja ya msaada wa kurudisha shukrani kwa
jamii katika kuelekea kilele cha kuadhimisha na kusherehekea miaka saba
(07) ya kutoa Huduma za mawasiliano hapana nchini pamoja na kuunga
mkono jitihada za serikali kupitia Sekta ya Afya katika kukabiliana na
changamoto ya uhaba wa damu katika hospitali au vituo vya kutolea huduma
za afya.
Daktari
wa dawa za usingizi katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI),
Bw; Juma Said Kabelele akiongea na waandishi wa Habari leo katika Ofisi
za makao Makuu Halotel wakati wa zoezi la uchangiaji damu
lililoendeshwa na Kampuni ya simu ya Halotel pamoja na Wafanyakazi kwa
kushirikiana na Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) ikiwa ni moja
ya msaada wa kurudisha shukrani kwa jamii katika kuelekea kilele cha
kuadhimisha na kusherehekea miaka saba (07) ya kutoa Huduma za
mawasiliano hapana nchini pamoja na kuunga mkono jitihada za serikali
kupitia Sekta ya Afya katika kukabiliana na changamoto ya uhaba wa damu
katika hospitali au vituo vya kutolea huduma za afya.
Afisa Masoko Kitengo Halopesa Roxana Christopher Kadio akishiriki
katika zoezi la uchangiaji damu lililoendeshwa na Kampuni ya simu ya
Halotel pamoja na Wafanyakazi kwa kushirikiana na Taasisi ya Tiba ya
Mifupa Muhimbili (MOI) ikiwa ni moja ya msaada wa kurudisha shukrani kwa
jamii katika kuelekea kilele cha kuadhimisha na kusherehekea miaka saba
(07) ya kutoa Huduma za mawasiliano hapana nchini pamoja na kuunga
mkono jitihada za serikali kupitia Sekta ya Afya katika kukabiliana na
changamoto ya uhaba wa damu katika hospitali au vituo vya kutolea huduma
za afya.
Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Simu Halotel Bw: Thang Bui Van akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo katika
ofisi za Makao Makuu ya Halotel leo katika zoezi la uchangiaji damu
lililoendeshwa na Kampuni hiyo pamoja na Wafanyakazi kwa kushirikiana na
Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) ikiwa ni moja ya msaada wa
kurudisha shukrani kwa jamii katika kuelekea kilele cha kuadhimisha na
kusherehekea miaka saba (07) ya kutoa Huduma za mawasiliano hapana
nchini pamoja na kuunga mkono jitihada za serikali kupitia Sekta ya Afya
katika kukabiliana na changamoto ya uhaba wa damu katika hospitali au
vituo vya kutolea huduma za afya.
Friday, October 7, 2022

Halotel yasherehekea miaka 7 ya utoaji huduma za Mawasiliano kwa kuchangia damu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment