BRELA WAFURAHISHWA NA MUITIKIO WA KUJISAJILI MAONESHO YA TATU UWEKEZAJI PWANI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 7, 2022

BRELA WAFURAHISHWA NA MUITIKIO WA KUJISAJILI MAONESHO YA TATU UWEKEZAJI PWANI

 Na Khadija Kalili, KIBAHA

MWANASHERIA wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Anneth Mfinanga amesema wamefurahishwa na mwitikio wa wafanya biashara na watu binafsi ambao wamefika kwenye banda lao katika maonesho ya tatu ya Uwekezaji na Biashara Mkoa wa Pwani 2022.

Mfinanga amesema hayo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo mchana kwenye maonesho hayo yanayoendelea kwenye viwanja vya stendi ya zamani ya mailimoja Kibaha Mkoani Pwani.

"Watu wengi waliojitokeza wamefanikiwa kupata vyeti vya usajili jambo ambalo linaleta hamasa" alisema Mfinanga.

"Tangu tumeanza maonesho haya Oktoba 5 licha ya mwamko pia kuna chagamoto ambazo zimejitokeza kwani wapo wafanya biashara ambao wamekua wakifanya biashara bila ya kujisajili na wamefika hapa ili kupata usajili ilhali wameshaanza biashara jambo ambalo tunapoingia kwenye mtandao tunakuta jina limeshasajiliwa huku mteja akilazimisha kutumia jina ambalo hajalisajili kwa sababu ya kuhofia kupoteza wateja hivyo nawasisitiza wafanyabiashara waje BRELA kujisajili kabla ya kuanza kufanya biashara"alisema Mfinanga.

Amezitaja huduma wanazozitoa ni pamoja na usajili wa alama za biashara, usajili wa makampuni , usajili wa majina ya biashara, usajili wa alama za biashara usajili na utoaji wa kusajili ubunifu.
wanasheri wa Wakala y Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Anneth Mfinanga  akizungumza na waandishi wa habari leo mchana kwenye maonesho hayo yanayoendelea kwenye viwanja vya stendi ya zamani ya mailimoja Kibaha Mkoani Pwani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad