WIKI moja kabla ya kufanyika
ya NMB Marathon ‘Mwendo wa Upendo,’ Benki ya NMB inayoandaa mbio hizo
imetangaza wadhamini zaidi ya 20, ambao wameeleza siri ya uamuzi wa
kukubali kudhamini kuwa ni kuguswa na wazo chanya la benki hiyo
kuwakomboa kinamama nchini.
Akizungumza wakati wa utambulisho huo
jijini Dar es Salaam jana, Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB, Juma Kimori,
aliwashukuru wadhamini hao kwa kusapoti mbio hizo na kurahisisha lengo
lengo la kukusanya Sh. Mil. 600 mwaka huu, hivyo kutoa nafasi mapato ya
miaka miwili ijayo ya mbio hizo kuyaelekeza katika maeneo mengine yenye
uhitaji.
Aidha, aliwataja Wadhamini Wakuu kuwa ni Sanlam Life
Insurance na UAP Insurance (Executive), huku Jubilee General Insurance
(ikiwa kategori ya Gold). Wadhamini wa kundi la Bronze ni pamoja na
Alliance Life Assurance, Britam Insurance Tanzania, Reliance Insurance,
ARiS Risk and Insurance Solutions na Metropolitan Life Insurance.
Wengine
wa kundi hilo ni pamoja na, huku Toyota, TBL, Strategis, Serena Hotel,
Azam, na Johari Rotana Hotel wakiwa ni miongoni mwa wadhamini wengineo.
Katika
kategori ya vyombo vya habari washirika, Kimori aliitaja EFM Radio, TV
E, Mwananchi Communications Limited, IPP Media na Almasi Productions,
orodha ilikamilishwa na Kampuni za SGA Security Tanzania, Gelato na
Grano Coffee.
Lakini pia, wadhamini hao waliipongeza NMB kwa wazo
chanya la kulikomboa kundi la kinamama wanaoshindwa kujitibu Fistula
kutokana na gharama kubwa na kwamba kujitokeza kwao kuunga mkono jambo
hilo, ni uthibitisho kwamba afya ya mama ni kipaumbele muhimu kwa jamii.
NMB
Marathon 2022, zinazolenga kukusanya kiasi cha Sh. Mil. 600 za kusaidia
matibabu ya kina mama wenye matatizo la Fistula wanaotibiwa kwenye
Hospitali ya CCBRT, zitafanyika Oktoba 1 kwenye viwanja vya Leaders
Club, Mgeni Rasmi akiwa ni Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa.

No comments:
Post a Comment