HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 22, 2022

Tarura- Bado Kuna uelewa mdogo juu ya ujenzi wa Madaraja kwa kutumia na teknolojia ya mawe na tofali za kuchoma


Mhandisi Mtaalamu wa Ujenzi wa Madaraja kwa kutumia Mawe Mhandisi Pharesi Ngeleja akizungumza na waandishi wa habari leo.
Moja ya Madaraja ya Mawe yaliyojengwa na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (Tarura) Kama linavyoonekana pichani.

Na Mwandishi Wetu Michuzi Tv
WAKALA wa Barabara za vijijini na Mijini (Tarura) umesema kuwa bado Kuna uelewa mdogo wa Wananchi na baadhi ya viongozi juu ya ujenzi wa Madaraja kwa kutumia na teknolojia ya mawe na tofali za kuchoma.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dodoma na Injinia Victor Seif Mtendaji Mkuu wa Tarura, alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari juu ya ubora na uimara wa teknolojia mpya ya Ujenzi wa Madaraja kwa kutumia Mawe na Tofali.

Injinia Seif amesema Tarura imeanza Ujenzi wa Madaraja kwa kutumia teknolojia ya mawe na Tofali lakini bado kumekuwa na uelewa mdogo kwa baadhi ya Wananchi na viongozi wa kisiasa katika Maeneo ya mradi.

"Sisi Kama Tarura tumeweza kuja na Teknolojia hii ambayo imekuwa ikipunguza gharama kubwa za Ujenzi kwa zaidi ya asilimia 50% kuliko ukitimia Nondo na saruji" Amesema Injinia Seif.

Ametaja kuwa katika Mkoa wa Kilimanjaro walitenga zaidi ya Milioni 400 kwa ajili ya Ujenzi wa Daraja moja kwa kutumia nondo na saruji lakini walivyoamua kutumia teknolojia ya mawe fedha hiyo imeweza Kujenga madaraja matatu zaidi.

Amesema kuwa Ujenzi huo ni rahisi kwakuwa unafanyika katika Maeneo ambayo Kuna mawe hivyo serikali inakuwa gharama yake ni saruji na utaalamu kutoka Kwa Wahandisi wa Tarura.

Ametaja kuwa Kuna Baadhi ya maeno wamekuwa wakiwatumia hata Mafundi wa kawaida na kuwafundisha namna ya Kujenga barabara na Madaraja kwa kutumia Mawe.

Injinia Seif ametaja kuwa mpaka sasa ni zaidi km 20 za barabara zimejengwa kwa mawe mkoani Mwanza huku km Zaidi ya 40 zikiwa zimejengwa mkoani Kigoma.

Kwa upande wake Mhandisi Mtaalamu wa Ujenzi wa Madaraja kwa kutumia Mawe Mhandisi Pharesi Ngeleja ametoa wito kwa Tasisi mbalbali za Ujenzi kujitokeza kwa winginkujifunza teknolojia hiyo kutoka Tarura.

Amesema Tasisi Kama Tanroad na zingine zikiweza kutumia mfumo huo utaokoa gharama za Ujenzi kwq zaidi ya asilimia 50% na kutaja kuwa Madaraja ya Mawe yameonyesha kuwa yanaishi muda mrefu kuliko ya nondo na saruji.

Ametaja kuwa Madaraja yote yaliyopo katika Reli nyakati yalijengwa kwa teknolojia hiyo na mpaka leo bado yanatumika na hayajaonesha kuchoka.
Mtendaji Mkuu wa Tarura, Victor Seif Mtendaji Mkuu wa Tarura, alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dodoma Leo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad