PROF.MAKUBI:ONGEZENI KASI YA UCHUNGUZI MIPAKANI KUZUIA EBOLA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 29, 2022

PROF.MAKUBI:ONGEZENI KASI YA UCHUNGUZI MIPAKANI KUZUIA EBOLA

 Na.Faustine Gimu ,Bukoba Kagera.

KATIBU mkuu wizara ya Afya Prof.Abel Makubi ametoa maagizo ya kuongeza kasi ya uchunguzi katika mipaka ya nchi katika mapambano ya Ugonjwa wa Ebola.

Prof.Makubi amebainisha hay oleo Septemba 29,2022 Wilayani Bukoba Mkoani wakati akizungumza na watumishi hospitali ya rufaa ya Bukoba mkoani Kagera mara baada ya kufanya ziara maeneo ya mpakani Mtukula kukagua hatua mbalimbali za serikali ambazo zimeshaanza kuchukuliwa katika kukabiliana na Ebola ili usienee nchini baada ya kuripotiwa visa vya ugonjwa huo nchi jirani ya Uganda hivi karibuni.

Aidha ,Prof.Makubi ameendelea kusisitiza kuwa hadi sasa hakuna visa vya ebola hata kimoja vilivyoripotiwa hapa nchini.

“Kwa sababu kuna njia nyingi za kupita wananchi katika mipaka nitoe maelekezo kuhakikisha kuongeza kasi ya uchunguzi katika mipaka tunaona kuna mipaka mingi wananchi wanapita.

Kuhusu suala la Uelimishaji pamoja na kuweka vifaa muhimu vya kupimo vya Ebola Prof.Makubi amesema wizara ya Afya imejipanga ambapo jopo la wataalam wizara Afya Kwa kushirikiana na wataalam wa afya kutoka mikoa ya mipakani ikiwemo Kagera wameendelelea kutoa elimu ambapo ameagiza kuongeza kasi ya uelimishaji zaidi kwa njia ya vyombo vya habari na vipeperushi mbalimbali.

“Serikali imejipanga kuhakikisha ugonjwa wa Ebola hauenei nchini na niwahakikishie watanzania hakuna Ebola Tanzania ,hatua ambazo zimeshaanza kuchukuliwa ni pamoja kusambaza vifaa vya kupimia Ebola na Ambulance “amesema.

Hivyo,Katibu mkuu huyo wa Wizara ya Afya amesisitiza kuendelea kuzingatia kanuni za afya ikiwemo kunawa mikono mara kwa mara.

Nao baadhi ya Wananchi mkoani Kagera akiwemo Fresta Abdallah,Khadija Rasuli pamoja na Ale Thomas wameishukuru serikali kwa kuendelea kuweka mikakati mbalimbali ya kukabiliana na Ebola huku wakiomba ukaguzi kuendelea kuimarishwa zaidi sehemu za mipaka.

MWISHO.
No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad