Phnom Penh, Cambodia – Septemba 20, 2022
Waandaaji
wa Tuzo za Kimataifa za Mitaji kwa Wajasirimali wadogo na wa Kati kwa
kushirikiana na Nchi za G20, Shirika la IFC (mwanachama wa Benki ya
Dunia) pamoja na Jukwaa la Kufadhili Ujasiriamali (SME Finance Forum)
mwaka huu wameanzisha kipengele kipya cha Hati Fungani Endelevu ya Mwaka
kuzitunuku Taasisi zinazofanya vizuri kwenye eneo hilo.
Hati
Fungani ya NMB JASIRI ndiyo imechaguliwa kama mshindi wa kwanza wa tuzo
hiyo mpya. Ushindi huo umepatikana baada ya Hati Fungani hiyo kupitiwa
na jopo la majaji zaidi ya 100 waliovutiwa na mlengo wake, muundo na
uwezo wa kulihudumia kifedha kundi ambalo halizingatiwi kwa Mitaji ya
kawaida iliyozoeleka.
Chanzo hiki cha Mtaji kinaendana vyema na
Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa na Kanuni za Dhamana
za Kijamii za Chama cha Kimataifa cha Masoko ya Mitaji.
Katika
hotuba yake ya kukubali tuzo na heshima hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa
Benki ya NMB, Bi Ruth Zaipuna, alisema: “Sisi NMB tumejitolea
kuhakikisha tasnia ya fedha inachangia maendeleo ya Tanzania. Hati
Fungani ya JASIRI yenye lengo la kupunguza pengo la Mitaji
linalozikabili biashara ndogo ndogo na za kati zinazomilikiwa au
kusimamiwa na akinamama ni keielelezo kizuri cha dhamira hii.”
Hati
Fungani yetu imefanikiwa kupata matokeo yaliyotarajiwa ya kusaidia
kuwawezesha wanawake kiuchumi na kushughulikia madhumuni matatu ya
Malengo ya Maendeleo Endelevu ambayo ni lengo la kwanza, la tano na la
kumi.
“Tuzo hii ni wakati muafaka wa kihistoria kwa sekta ya
benki nchini, kwani inaiweka nchi yetu katika ramani ya dunia kwa
uongozi kwenye Mitaji endelevu. Hati Fungani ya JASIRI inaweka kigezo
kipya nchini na barani Afrika katika kukuza vyanzo vingine vya Mitaji
mbadala kwa ajili ya wawekezaji wa ndani na wakimataifa,” aliongeza.
Bi
Zaipuna amesema tuzo hiyo ni kwa ajilia wa wafanyakazi wote wa NMB,
washirika wake, wawekezaji na wasimamizi wa sekta ya fedha kwa kuchangia
mafanikio makubwa ya dhamana ya JASIRI.Mhazini
wa Benki ya NMB – Aziz Chacha (Kushoto) akipokea tuzo ya Hati Fungani
Bora ya Mwaka 2022 kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Jukwaa la Ufadhili
wa Ujasiriamali (SME Finance Forum) – Mathew Gamser kwenye hafla ya tuzo
iliyoandaliwa na Waandaaji wa Tuzo za Kimataifa za Mitaji kwa
Wajasirimali Wadogo na wa Kati kwa kushirikiana na Nchi za G20, Shirika
la IFC(mwanachama wa Benki ya Dunia) pamoja na Jukwaa la Kufadhili
Ujasiriamali (SME Finance Forum) jijini Phnom Penh, Cambodia. Benki ya
NMB kupitia hatifungani yake ya NMB Jasiri imeshinda tuzo ya ‘Platinum’
Upande wa Kundi la Dhamana Endelevu ya Mwaka Kwenye Tuzo za Ufadhili wa
Ujasiriamali za Mwaka 2022.
No comments:
Post a Comment