KUTOKANA na wakusanya kodi
kukabiliwa na changamoto ya kujua viwango vya kweli vya kodi kwa
uzalishaji uliopo, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilifikiria kutafuta
njia nyingine ya kisasa na sahihi ili kukabiliana na changamoto hiyo.
Kazi
ya kupata mfumo sahihi kukabiliana na changamoto hiyo ilipewa kampuni
ya Uswisi, ya Société Industrielle et Commerciale de Produits
Alimentaires (SICPA). Kampuni hii ilikuja na mfumo wa stempu wa
kielektroniki (ETS).
Kufanikisha utendaji wakeTRA iliweka awamu
kadhaa za utekelezaji wa mfumo, ambapo katika awamu ya kwanza ya mfumo,
iliyozinduliwa Januari 15,2019 stempu za kielektroniki ziliwekwa kwa
kampuni 19 zinazozalisha bidhaa za pombe, mvinyo na vinywaji vikali
nchini.
Awamu ya pili ya stempu za kielektroniki iliyoanza
Agosti 1,2019 ziliwekwa kwenye bidhaa kama vile maji yaliyotiwa ladha
tofauti na kwenye vinywaji vingine visivyo vya kileo.
Katika
mahojiano Meneja Miradi wa TRA wa Mfumo wa ETS, Innocent Minja anasema
lengo kuu la kutafuta mfumo mpya wa ukusanyaji kodi na uzinduzi wa ETS
miaka mitatu iliyopita ni kulinda mapato ya serikali.
"Tulikuwa
na changamoto kubwa ya ukusanyaji wa kodi kutokana na watu kutokuwa wa
kweli na pia uwapo wa uzito katika ulipaji kodi kwa hiari.
“Awali
tulilazimika kuweka maofisa wetu kuangalia uzalishaji na kuhakikisha
watengenezaji wanatangaza viwango vya kweli vya uzalishaji. Hata hivyo,
hali hiyo ilikuwa na changamoto nyingi na kuonekana kama vurugu
tukahitaji suluhu mpya,” anasema Minja.
Minja anasema kutokana
na baadhi ya wazalishaji kutokuwa wakweli kuhusu uzalishaji wao na hivyo
kusababisha ushindani usio wa haki wa bidhaa zao sokoni na wale
wanaosema kweli na kulipa kodi stahiki.
Minja anasema kwamba
mfumo wa ETS katika kipindi cha miaka mitatu umeimarisha ulipaji wa kodi
na hivyo kuimarisha ushindani wa haki sokoni.
"Hii imesababisha kila mtengenezaji wa bidhaa iliyomo kwenye mfumo kulipa kodi kwa haki," anasema Minja.
Ufungaji wa ETS umehakikisha kuwa TRA inapata data za uzalishaji kwa wakati (muda halisi) kutoka kwa watengenezaji.
"Hii
ni kwa sababu ya kodi ya ushuru kwa bidhaa maalumu hutozwa kwa kwango
cha uzalishaji hiyo kujua takwimu za uzalishaji ni muhimu."
Kama
ilivyotarajiwa, kuanza kwa mfumo wa ETS uliambatana na uwapo wa vifungo
vya usalama kwenye teknolojia husika na kurahisisha usimamizi wa kodi
nchini.
“ Mfumo ulileta uwazi kwenye kodi hasa kwenye kodi ya
ushuru, Kodi ya ongezeko la thamani (VAT) na kodi ya kampuni na hatimaye
kupunguza manung’uniko ya walipa kodi,” anasema Minja.
Anasema mchakato wa ufungaji ni endelevu haswa kutokana na viwanda kuendelea kuongeza viwango vya mitambo yao.
"Tayari
tumeweka mfumo wa ETS kwa watengenezaji wote wanaostahiki wa bidhaa
maalum. Takriban vifaa 135 vimefungwa kwenye viwanda vyenye mitambo
inayojiendesha huku viwanda visivyojiendesha vikilazimika kuwasha mfumo
huo kila wanapoanza uzalishaji,” anasema Minja.
Pamoja na
kufanikisha uwekezaji wa mfumo mfumo wa ETS; mfumo huo umekuwa ni msaada
mkubwa kwa wazalishaji na waingizaji wa bidhaa mbalimbali.
Mfumo
huo pia umewezesha wazalishaji wa bidhaa kujua kiasi cha bidhaa
zinazoingizwa sokoni kutoka nje, hivyo kusaidia kuwapatia taarifa
wazalishaji wa ndani nini wakifanye ili kuhami bidhaa zao sokoni dhidi
ya zile zinazotoka nje.
"Mfumo huu umeongeza uwazi, na kwa sasa,
watengenezaji na waagizaji wa bidhaa zilizomo kwenye mfumo
wanahakikishiwa usawa sokoni kwa kuwa kila mtu analipa ushuru wa kweli
na sahihi wa bidhaa husika na kinyume na awali kabla ya mfumo."
Aliongeza
kwamba ETS sio tu imerahisisha kadirio la makusanyo ya kodi, lakini pia
mfumo umesaidia wazalishaji kutambua kiasi cha uzalishaji na muda
ulitumika kuzalisha bidhaa husika. Pia imesaidia kujua changamoto
zinazohusiana na mchakato wa uzalishaji na kutafuta suluhu za changamoto
hizo. ETS ikitumika vizuri kwa usahihi malipo ya VAT pia yanakuwa
sahihi na pia kurahisisha ukusanyaji na ulipaji wa kodi.
Pamoja
na ufanisi uliowezeshwa na mfumo huo, TRA imesema imekuwa ikikabiliana
na baadhi ya wafanyabiashara ambao wamekuwa wakitumia stempu za
kughushi.
“Tunawaomba wazalishaji, waagizaji na wananchi kwa
ujumla, kutumia kwa dhati mfumo huo na kuepuka matumizi ya stempu za
kughushi,” anasema Minja na kuongeza kuwa TRA inafuatilia kwa makini
ufanisi wa mfumo huo pote nchini.
Kwa mujibu wa Minja Mamlaka
huendesha kampeni kampeni za mara kwa mara kuelimisha wafanyabiashara
jinsi ya kuzitambua stempu hizo za kugushi.
Afisa
wa TRA, Bw. Chama Siriwa akitoa elimu kwa wananchi na kuhamasisha
kutumia App ya Hakiki Stempu na kupakua app hiyo katika simu zao ili
waweze kuhakiki vinywaji kabla ya matumizi.
Maofisa
wahamasishaji wa program ya ETS - Hakiki Stempu wakitoa elimu kwa
wafanyabiashara katika zoezi linaloendelea la kuhamasisha matumizi ya
App hiyo katika sehemu mbalimbali nchini.
Tuesday, September 20, 2022
KWANINI MFUMO WA ETS NI SAHIHI KATIKA UKUSANYAJI WA KODI.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment