KATIBU MKUU MAGANGHA AONGOZA KIKAO CHA MRADI WA KIMAZINGIRA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 30, 2022

KATIBU MKUU MAGANGHA AONGOZA KIKAO CHA MRADI WA KIMAZINGIRA

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati Tendaji ya Kitaifa ya Mradi mradi wa kujenga uwezo wa utayari wa nchi kuhimili athari za Mabadiliko ya Tabianchi kupitia Kuandaa Mpango wa Taifa wa Kuhuisha Masuala ya Kuhimili Athari za Mabadiliko ya Tabianchi Katika Mipango ya Nchi mara baada ya kufanyika kikao hicho leo Septemba 30, 2022 jijini Dodoma.


Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga akiongoza Kikao cha Kamati Tendaji ya Kitaifa ya Mradi mradi wa kujenga uwezo wa utayari wa nchi kuhimili athari za Mabadiliko ya Tabianchi kupitia Kuandaa Mpango wa Taifa wa Kuhuisha Masuala ya Kuhimili Athari za Mabadiliko ya Tabianchi Katika Mipango ya Nchi kilichofanyika leo Septemba 30, 2022 jijini Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)


Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga ameongoza Kikao cha Kamati Tendaji ya Kitaifa ya Mradi mradi wa kujenga uwezo wa utayari wa nchi kuhimili athari za Mabadiliko ya Tabianchi kupitia Kuandaa Mpango wa Taifa wa Kuhuisha Masuala ya Kuhimili Athari za Mabadiliko ya Tabianchi Katika Mipango ya Nchi.Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma leo Septemba 30, 2022 kimehusisha wajumbe kutoka Wizara za kisekta, sekta binafsi na Asasi za Kiraia

Lengo la mradi huo ni kuimarisha uwezo wa nchi katika kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi kwa kujumuisha, masuala ya mabadiliko ya tabianchi katika mipango ya maendeleo.

Mradi utawezesha wizara na taasisi kuwa na mipango ya kuhimili mabadiliko ya tabianchi na kuimarisha uratibu wa taasisi na wadau husika katika kutekeleza mipango ya uhimilivu na maendeleo ili kuimarisha ukusanyaji wa takwimu kutoka katika sekta zinazoathiriwa zaidi na mabadiliko ya tabianchi.

Aidha, matokeo tarajiwa ya utekelezaji wa mradi yanatarajiwa kuwa ni kuboresha uwezo wa kitaifa wa upangaji wa mipango ya kuhimili mabadiliko ya tabianchi na kuimarika kwa uratibu wa taasisi na wadau.

Pia kuimarisha ukusanyaji wa takwimu kutoka katika sekta zinazoathiriwa zaidi na mabadiliko ya tabianchi pamoja na Mpango wa Taifa wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi kuandaliwa na kupitishwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad