HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 8, 2022

DKT.MWINYI AMEMUAPISHA MKURUGENZI MKUU MPYA WA ZAECA

 


Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abduulla (kushoto) Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe.Khamis Ramadhan Abdalla na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Mkurugenzi Mkuu wa Zaeca Bw,Ali Abdalla Ali katika Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo.
Viongozi Wakuuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wakipiga saluti wakati Wimbo wa Taifa ukipigwa leo kabla ya kuapishwa Mkurugenzi Mkuu Mpya wa ZAECA Bw.Ali Abdalla Ali (kulia) hafla ya kiapo imefanyika Ukumbi wa Ikulu Jijini Zazibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akimkabidhi Hati ya kiapo Nd. Ali Abdalla Ali mara baada ya kumuapisha kuwa Mkurugenzi Mkuu wa ZAECA,hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) alipokuwa akizungumza na Viongozi mbali mbali (hawapo pichani) waliohudhuria katika hafla ya kumuapisha Nd. Ali Abdalla Ali kuwa Mkurugenzi Mkuu wa ZAECA,hafla iliyofanyika Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar pamoja na kutoa maelekezo maalum kwa Mkurugenzi huyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) alipokuwa akimkabidhi Vitabu Nd.Ali Abdalla Ali, ikiwa ni muongozo katika utekelezaji wa kazi zake mara baada ya kumuapisha kuwa Mkurugenzi Mkuu wa ZAECA,katika hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad