HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, September 24, 2022

BancABC yazindua kampeini kwa wateja wa akaunti za amana

 

 
-Wateja wanaoufungua akaunti za amana kupata riba hadi asilimia 11 papo hapo

BancABC Tanzania ambayo ni kampuni tanzu ya Atlas Mara na ambao imeorodhesha kwenye soko la hisa la London, imepiga hatua nyingine kwenye soko baada ya kuzindua kampeini maalum inayolenga kuwanufaisha wateja wanaofungua akaunti za amana.

Kwenye kampeini hiyo ambayo inaanza leo na kuendelea mpaka Disemba 15 mwaka huu, wateja wa BancABC Tanzania watakaofungua akaunti za amana watapata riba ya hadi asilimia 11 papo hapo.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kuzindua kampeini hiyo, Afisa Mkuu Muendeshaji BancABC Tanzania Joyce Malai alisema kuwa benki hiyo imezindua kampeini ambapo wateja wanaofungua akaunti za amana watapata riba ya asilimia 11 kuanzia leo mpaka katikati ya mwezi Disemba mwaka huu. Riba hiyo italipwa papo hapo huku salio ya akaunti ikiendelea kubaki salama mpaka muda wa ukomavu atakapofika.

‘Hii ni moja ya ofa bora kabisa kwenye soko na naomba kutumia hii fursa kuwaomba wateja wetu na Watanzania ambao hawana akaunti na sisi kutumia nafasi ili kufaidika na kampeini hii’, unavuna kabla ya kupanda, alisema Malai.

Malai alisema kuwa BancABC imejidhatiti kufikia mahitaji ya wateja na kuhakikisha kwamba wanakua pamoja na benki hiyo. “Tunathamini jinsi wateja wetu wanavyotuunga mkono na hiyo ndio sababu sisi kama benki tumeamua kuwazawadia ofa hii kabambe’.

Aliongeza kuwa BancABC ipo tayari kukubali wateja kufungua akaunti za amana kwa kipindi cha robo ya mwaka, nusu au mwaka na riba italipwa papo hapo kwa akaunti zote hizo. ‘Sisi kwetu mteja ni mfalme na ndio sababu tuko tayari kusikiliza’, Malai alisema.

Kwa upande wake, Meneja wa Kitengo wa Wateja wa Rejareja na Biashara Lillian Mwakitalima alisema kuwa kinachotakiwa kufanywa na mteja yeyote ili aweze kujipatia ofa hii nikufika kwenye matawi yetu nchini kote na kufungua akaunti ya amana ya muda maalumu ambapo riba hiyo italipwa papo hapo, lengo ni kukupa uhuru wa wa kupanga kwa sasa au kwa baadae.

‘Mteja anapaswa kutembelea tawi lolote la BancABC Tanzania na kufungua akaunti ya amana na riba yake kulipwa hapo hapo, na mteja anaweza kutumia riba kwa kufanya manunuzi, kufanya matembezi au kuwanunulia zawadi wanafamilia au marafiki’, Mwakitalima aliongeza.

‘Mteja pia anaweza kutumia akaunti hii ya amana kupata mkopo. Tunakaribisha wateja watutembelee kwani sisi tuko huru kuwasikiliza’, alisema Mwakitalima huku akiongeza kuwa mteja anaweza kuwasiliana nasi kwa kupiga 0779 111000 au kutembelea moja ya matawi yetu waliopo Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza na Arusha kasha kufungua akaunti ya amana na kuanza kufaidika mara moja.


Meneja wa Kitengo wa Wateja wa Rejareja na Biashara BancABC Tanzania Lillian Mwakitalima (kushoto) akizungumza jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki baada ya kuzindua kampeini maalum inayolenga kuwanufaisha wateja wanaofungua akaunti za amana ambapo kwenye kampeini hiyo ambayo inaanza leo na kuendelea mpaka Disemba 15 mwaka huu, wateja wa BancABC Tanzania watakaofungua akaunti za amana watapata riba ya hadi asilimia 11 papo hapo. Kulia ni Afisa Mkuu Muendeshaji BancABC Tanzania Joyce Malai.

Meneja wa Kitengo wa Wateja wa Rejareja na Biashara BancABC Lillian Mwakitalima (kushoto) akiwa na Afisa Mkuu Muendeshaji BancABC Tanzania Joyce Malai (kulia) wakionyesha bango mara baada ya kuzindua kampeini maalum inayolenga kuwanufaisha wateja wanaofungua akaunti za amana ambapo kwenye kampeini hiyo ambayo inaanza leo na kuendelea mpaka Disemba 15 mwaka huu, wateja wa BancABC Tanzania watakaofungua akaunti za amana watapata riba ya hadi asilimia 11 papo hapo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad