HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 13, 2022

BALOZI WA TANZANIA NCHINI INDONESIA AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO

 BALOZI wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Indonesia Mhe. Macocha Tembele mapema leo tarehe 13/09/2022 amewasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais wa Indonesia Mhe. Joko Widodo katika hafla iliyofanyika kwenye Kasri la Merdeka jijini Jakarta. 

 

Katika hafla hiyo, wawili hao walipata fursa  ya kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kuimarisha ushirikiano katika sekta ya biashara na uwekezaji. 

 

Hatua hiyo ya  Mhe. Balozi Makocha Tembele kuwasilisha hati zake za utambulisho inaashiria kuanza rasmi kwa utumishi wake katika nchi hiyo.  

Balozi wa Tanzania nchini Indonesia Mhe. Macocha Tembele akiwasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais wa Nchi hiyo Mhe. Joko Widodo

  Balozi wa Tanzania nchini Indonesia Mhe. Macocha Tembele akisalimiana na Rais wa Nchi hiyo Mhe. Joko Widodo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad