Waziri
wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Mhe. Dkt.
Dorothy Gwajima ameipongeza benki ya NMB kwa kutenga fedha kwaajili ya
mikopo ya machinga na pia kuweka huduma zitakazorahisisha utendaji kazi
wa kundi hili la wafanyabiashara wadogo.
Waziri Gwajima
ameyaeleza hayo alipotembelea soko la machinga la old airport jijini
Mbeya na kujionea hali halisi ya Biashara za machinga katika soko hilo
ambalo machinga wamehamia tangu mwaka 2020.
Mhe waziri
aliipongeza benki ya NMB kwa kutenga kiasi cha Bilioni 200 kwaajili ya
kuwakopesha machinga jambo ambalo litawasaidia kujikwamua kiuchumi.
Naye
Mwenyekiti wa shirikisho la Umoja wa Machinga Tanzania (SHIUMA), Ndugu
Ernest Matondo Masanja aliishukuru Benki hiyo pia kwa kuanzisha rasmi
kadi za ATM maalumu kwa machinga huku akiwasihi machinga wote nchini
kuunga mkono juhudi za Benki hiyo kuwainua kiuchumi.
Lakini pia,
Meneja wa Benki ya NMB kanda ya Nyanda za Juu, Straton Chilongola
alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wamachinga kuwa licha ya huduma bora
ambazo NMB inatoa, lakini pia, wanaweza kujikatia bima mbalimbali
ikiwemo bima maalumu kwaajili ya Machinga ambayo itawafanya wafanye
shughuli zao kwa kujiamini na kutokuwa na hofu kwani itokeapo janga
lolote basi Bima itafidia.
Sunday, August 14, 2022

WAZIRI GWAJIMA AIPONGEZA NMB KUWAJALI MACHINGA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment