SERIKALI YATOA VISHIKWAMBI 270 KWA AJILI YA KUWAFUNDISHIA WANAFUNZI MASUALA YA ELIMU YA UZAZI NA KUJIKINGA NA VVU - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 4, 2022

SERIKALI YATOA VISHIKWAMBI 270 KWA AJILI YA KUWAFUNDISHIA WANAFUNZI MASUALA YA ELIMU YA UZAZI NA KUJIKINGA NA VVU

Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Paskas Muragili, akimkabidhi Kishikwambi Sr. Josephine Revelion kutoka Shule ya Musange.

Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Paskas Mragili, akizungumza na walimu jana wakati akiwakabidhi vishikwambi 270 ambavyo vitatumika katika shule 135 za msingi na sekondari kwa ajili ya kufundisha masuala ya elimu ya uzazi na jinsi ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Ester Chaula, akizungumza katika makabidhiano hayo.
Walimu kutoka wilaya hiyo wakisubiri kukabidhiwa Vishikwambi hivyo.
Vishikwambi vikikabidhiwa.


Mwalimu Pius Chigego akikabidhiwa Kishikwambi.

Na Dotto Mwaibale, Singida
MKUU wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Paskas Mragili, amezitaka shule za msingi na sekondari wikayani hapa kujipanga kuingia katika mfumo wa ufundishaji kwa njia ya kidigitali kwa kuwa mpango wa serikali ni kutaka utendaji wote uwe unafanyika kidigitali.

Alisema hayo jana baada ya kukabidhi walimu vishikwambi 270 ambavyo vitatumika katika shule 135 za msingi na sekondaji kwa ajili ya kufundisha masuala ya elimu ya uzazi na jinsi ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi.

"Mpango wa serikali ni kutaka kuhama kabisa katika utendaji wa 'analog' kwenda kwenye utendaji wa kidigitali hivyo lazima shule zijipange kuingia katika mfumo huo," alisema.

Mragili alisema anafahamu zipo shule zitakuwa ndio zinaanza kwa mara ya kwanza matumizi ya kidigitali katika ufundishaji hivyo ziwe mfano bora kwa zingine ili ziweze kuvutika kutumia teknolojia hiyo.

"Wengi wetu hapa mna simu za smartphone mnazitumia vizuri sasa kinachofanyika hapa umeongezewa ukubwa wa 'screen' tu kinachofanyika katika vishikwambi hivi ni sawa na simu tu ziadi hapa kilichongezewa ni programu maalum ya masomo haya," alisema.

Mragili alisema shule ambazo zimebahatika kupata vishikwambi hivyo ziwe mfano kutumia vifaa hivyo ili kuzivutia zingine kutumia teknolojia hiyo na shule zione umuhimu wa kuongeza vishikwambi zaidi kwani viwili ambavyo vimetolewa kwa kila shule havitoshelezi.

Alisema walimu lazima watambue kuwa mpango huu ulipoanzisha tayari tafiti ziliehafanyika na kuona kuna tatizo la elimu ya uzazi kwa vijana hivyo wahakikishe wanafundishwa ili waweze kujitambua na kupunguza maambukizi ya VVU.

"Naomba Singida tuwe miongoni mwa halmashauri zitakazofanya vizuri katika proramu hii ili kuwafanya vijana wawe na afya njema na wafikie ndoto zao katika maisha yao," alisema.

Mkuu huyo wa Wilaya alisisitiza suala la itunzaji wa vishikwambi hivyo ili visaidie vijana wengine zaidi na kwamba kuvifabya kuwa mali ya shule sio kwamba utunzani uwe wa kulegalega.

Aidha, aliishukru serikali kwa kutoa vishikwambi kwa kutoonyesha ubaguzj ambapo vimetolewa kwa shule za serikali na binafsi kwa suala la elimu ya afya huwezi kubagua kati ya wanafunzi wanaosoma shule binafsi na za serikali.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Ester Chaula, alisema vishikwambi hivyo vitatolewa kwa walimu 270 waliopewa mafunzo ya namna ya kuvitumia na vitakuwa mali ya shule.

Alisema halmashauri yake imekuwa miongoni mwa Halmashauri 20 kati ya 184 zilizogawiwa vishikwambi hivyo ambapo shule za msingi 94 na sekondari 41 ndizo wanafunzi wake watafundishwa masomo ya uzazi wa mpango na jinsi ya kujikinga na maambukizi ya VVU.

Alisema serikali imetoa vishikwambi hivyo ili kuweza kutoa elimu ya uzazi wa mpango na maambukizi ya VVU ili kufikia malengo ya mradi unaojulikana kama Timiza Malengo unaoendeshwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

Chaula alitoa wito kwa walimu pamoja na kwamba vishikwambi vimetolewa kwa ajili ya kufundishia masualanya elimu ya uzazi lakini pia vitaweza kutumika kufundisha masomo mengine kwasababu vina uwezo wa kuhifadhi 'materials' ya masomo mengine yanayofindishwa shuleni.

Alisema mwelekeo wa serikali ni kufanya kila kitu kufanyika kwa njia ya kidigitali ambapo kutumia teknolojia hii kutapunguza matumizi ya karatasi na wanafunzi watafundishwa elimu ya uzazi na jinsi ya kujikinga na maambukizi ya VVU kwa njia ya picha.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad