HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, August 20, 2022

Sensa ya Watu na Makazi maandalizi yake yamefikia asilimia 99-Balozi Hamza

 

Kamisaa wa Sensa upande wa Zanzibar Balozi Mohamed Haji Hamza akizungumza kuhusiana na maandalizi ya Sensa kuelekea Agasti 23 jijini Dar es Salaam kushoto ni Kamisaa wa Sensa  Spika Mstaafi Anne Semamba Makinda.
Mtakwimu Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt.Albina Chuwa akizungumza namna walivyojipanga na kamati Sensa kuelelekea Agasti 23, Jijini Dar es Salaam kushoto ni Kamisaa wa Sensa Upande wa Zanzibar Balozi Mohamed Haji Hamza.

*Viapo vya Makarani watakiwa kuzingatia ya kutotoa siri za kaya

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
KAMISAA wa Sensa ya Watu na Makazi kwa upande wa Zanzibar Balozi Mohamed Haji Hamza amewataka makarani wa sensa kutotoa siri za kaya wanazokwenda kukusanya taarifa hii ni kutokana na kiapo walichokula kabla ya kuanza mafunzo hayo.

Kutoa siri kwa karani wa Sensa kifungo cha miaka miwili hiyo kwa mujibu wa sheria ya takwimu.

Pia amesema hakuna mwananchi yeyote atakayefungwa kwa sababu ya kutotoa taarifa za sensa isipokuwa serikali ikipanga mipango wasiohesabiwa wakati wa utoaji huduma watachukua haki ya wengine waliohesabiwa.

Akizungumza jana Dar es Salaam, Balozi Hamza amesema jukumu la sensa lipo mabegani mwa makarani hivyo wanatakiwa kuwa waangalifu kwa kuwa limegharimu rasilimali ya Taifa nyingi katika kuandaa kwake hivyo makarani wanatakiwa kuwa makini na kufanya kazi kwa mujibu wa sheria.

Amesema maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi imefikia asilimia 99 ambapo Agasti 23 ni kwenda kutekeleza kutokana na maandalizi hayo

"Kila karani alipewa mkataba wake na aliusoma kwa umakini na alisaini hivyo haitakiwi kutoa siri yeyote ya kaya wakati wa kuchukua dodoso la sensa" amesema Balozi Hamza

Balozi Hamza alizitaka kaya zote nchini kutoa ushirikiano wa kutosha kwa makarani na wasimamizi wa sensa kwa kutoa taarifa sahihi kwa ajili ya maendeleo ya taifa.

Aidha alisema Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa sensa ya mwaka huu inafanyika kwa umakini katika kupata idadi ya watu itakayosaidia kupanga maendeleo.

Naye, Mtakwimu Mkuu wa Serikali Serikali Dk.Albina Chuwa alisema Oktoba mwaka huu,watatoa matokeo ya sensa hivyo watawahamasisha viongozikutumia data hiyo kwa ajili ya kupanga maendeleo.

"Huwezi kufanya maendeleo kama huna hesabu kamili ya wananchi lakini Oktoba mwaka huu ikishajulikana watanzania wapo wangapi shule,hospitali na vitu vyote vyenye umuhimu kwa jamii vitaongezwa"alisema Dkt.Albina.

Katika mkutano huo Dk.Albina alitaja idadi ya wasimamizi wa sensa ambao hadi sasa wapo 205,000 wamemaliza mafunzo kwa nadharia na vitendo.

Alisema katika sensa ya mwaka huu,maeneo ya kuhesabia watu ni 104,334 kati ya hayo Tanzania bara ni 100,003 na Zanzibar ni 4301.

Dk.Albina alitoa wito kwa makarani na wasimamizi wa sensa kuwa kuanzia leo wanatakiwa kilipoti ofisi za viongozi ya maeneo husika iliwemo kata,kijiji,,mtaa na kitongoji kujitambulisha kwa maeneo husika.

Amesema lengo lakufika kwa viongozi hao ni kutambua masuala mbalimbali katika eneo lake atakalo hesabu watu ikiwemo kujua kama kuna makundi maalumu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad