HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 19, 2022

RC MAKALLA ATANGAZA KIAMA KWA WAZALISHAJI MIFUKO YA PLASTIKI DSM, TBC, NEMC WATOA NENO

*Wazalishaji Mifuko mbadala waomba Serikali kuchukuwa hatua.

* NEMC na TBS Watoa tamko la kusimamia Operesheni, Wataka Mikoa ya mipakani kuimarisha Udhibiti.
* RC aagiza kuhitishwa kikao Cha Wenyeviti wa Masoko DSM.

MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo August 19 ametangaza Operesheni ya kukamata Mifuko ya plastic iliyokatazwa na kuwataka Wananchi kujiepusha na Matumizi ya Mifuko hiyo.

RC Makalla ametangaza Operesheni hiyo wakati wa kikao kazi Wazalishaji Mifuko mbadala, Kamati ya Ulinzi na usalama na Mamlaka za Udhibiti ikiwemo TBS na NEMC Baada ya kubaini Mifuko iliyokatazwa imeanza kurudi upya.

Aidha RC Makalla ameagiza kuhitishwa kikao Cha Wenyeviti wa Masoko yote ya Mkoa huo na kutolewa maelekezo ya katazo la uuzaji wa Mifuko iliyokatazwa kwenye Masoko yao.

Pamoja na hayo RC Makalla ameelekeza Mamlaka ya Udhibiti na usimamizi wa Mazingira NEMC kurudi upya kutoa Elimu kwa Wananchi kuhusu Madhara ya Matumizi ya Mifuko hiyo.

Miongoni mwa Madhara ya Matumizi ya Mifuko iliyokatazwa ni Uchafuzi wa Mazingira, Ukwepaji wa Kodi Kutokana na Mifuko Kuuzwa kinyemela pamoja na kuua viwanda vilivyopewa kazi ya kuzalisha Mifuko mbadala.

Kwa upande wao Mamlaka za Udhibiti kupitia Wakurugenzi wa NEMC na TBS wametumia kikao hicho kutoa tamko la kusimamia Operesheni hiyo ambapo wamemuahidi RC Makalla kuwa Operesheni hiyo itafanikiwa.

Wazalishaji wa Mifuko mbadala wamekiri uzalishaji wa Mifuko iliyoruhusiwa kudorora Kutokana na kuzagaa kwa Mifuko iliyokatazwa kwenye Masoko na Maduka jambo linalopelekea viwanda vyao kufa ambapo wameiomba Serikali kusimamia Operesheni hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad