HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 26, 2022

RAIS WA ZANZIBAR AJUMUIKA NA WAUMINI WA DINI YA KIISLAM KATIKA SALA YA IJUMAA MASJID NABAWI MBUYU MNENE LEO

 

Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwasalimia Watoto baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Masjid Nabawi Mbuyu Mnene Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 26-8-2022.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa zawadi ya Ayatul Kursiyu na Kiongozi wa Masjid Nabawi Sheikh Ali Aboud,baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Masjid hiyo iliyoko katika mtaa wa Mbuyu Mnene Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo. 26-6-2022.
Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na hundi ya shilingi laki tano iliyotolewa Sadaka na Uongozi wa Masjid Nabawi, kwa ajili ya kusaidili shughuli za Kijamii, akimsikiliza Kiongozi wa Masjid hiyo Sheikh Ali Aboud, baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika leo 26-8-2022.
Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuwasalimia Wananchi wa Masjid Nabawi Mbuyu Mnene Wilaya ya Magharibi “B” Unguja, baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Masjid hiyo leo 26-8-2022.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Waumini wa Kiislam katika kuitikia dua ikisomwa na Sheikh Ali Mohammed Ali.(hayupo pichani) baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Masjid Nabawi Mbuyu Mnene Wilaya ya Magharibi “B”Unguja leo 26-8-2022.(Picha na Ikulu)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad