HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, August 9, 2022

PARIMATCH KUDHAMINI MBEYA CITY KATIKA MICHUANO YA LIGI KUU TANZANIA BARA

 

Afisa Mtendaji wa timu ya Mbeya City, Emmanuel Kimbe akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 9,2022 jijini Dar e Es Salaam wakati wa kutambulisha mkataba wa makubaliano PariMatch katika Michuano ya ligi kuu Tanzania Bara msimu wa 2022/2023.

Afisa Habari wa PariMatch Tanzania, Ismail Mohamed akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 9,2022 jijini Dar e Es Salaam wakati wa kutambulisha mkataba wa makubaliano na Timu ya Mbeya City katika Michuano ya ligi kuu Tanzania Bara msimu wa 2022/2023. Katikati ni Afisa Mtendaji wa timu ya Mbeya City, Emmanuel Kimbe na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa PariMatich Tanzania, Ruby Chuku.
Mkurugenzi wa Masoko wa PariMatich Tanzania, Ruby Chuku akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo baada ya kuingia makubaliano ya udhamini wa Ligi kuu Tanzania Bara katika msimu wa 2022/2023. kulia ni Afisa habari Manispaa ya Mbeya, John Kilua na Kushoto ni Afisa Mtendaji wa timu ya Mbeya City, Emmanuel Kimbe

Na Avila Kakingo, Michuzi TV
KAMPUNI ya Michezo ya Kubashiri Mtandaoni hapa nchi ya PariMatch imeingia makubaliano na Timu ya Mpira wa Miguu inayomilikiwa na jiji la mbeya 'Mbeya City'.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 9,2022 jijini Dar e Es Salaam Afisa Habari wa PariMatch Tanzania, Ismail Mohamed amesema kuwa udhamini huo utakuwa katika michuano ya ligi kuu Tanzania Bara kwa msimu wa 2022/2023.

Mohamed amesema kuwa Mkataba huo utakuwa na faida kwa pande zote mbili kati ya kampuni hiyo na Timu inayoshiriki ligi kuu ya Mbeya City.

Akizungumzia sababu ya kudhamini Mbeya City amesema kuwa idadi ya Mashabiki na ushawishi wa Soka hapa nchini ndio uliopelekea kurejea tena kudhamini timu hiyo kwa msimu huu mpya.

"Sisi Parimatch moja ya jukumu letu ni kuhakikisha michezo inakua kuanzia ngazi ya chini hadi ngazi ya Kimataifa." Amesema Mohamed

Amesema wanaendelea kuunga mkono vilabu vingine katika ligi kuu, dalaja la kwanza ba hata vilabu chipukizi.

"Tunaunga mkono juhudi za TFF na bodi ili kuhakikisha ligi za Tanzania zinakuwa za Kimataifa." Amesema Mohamed

Kwa Upande wa Afisa Mtendaji wa timu ya Mbeya City, Emmanuel Kimbe amewashukuru PariMatch kwa udhamini walioutoa na kuendelea kushirikiana nao katika kukuza soka la hapa nchini.

"Tunashukuru sana kwa kuwa pamoja tena katika msimu huu maana msimu uliopita hatukuwa pamoja, tuwaahidi ushirikiano kwaniaba ya wanambeya wote." Amesema Kimbe

Afisa habari Manispaa ya Mbeya, John Kilua amesema kuwa PariMatch waendelee kuwaamini na Mbeya City na watawapa kile kinachostahili na kile kinachotarajiwa.

"Nafahamu PariMatch mnahitaji kuona Perfomance ya timu inakuwa nzuri, tunajua nini mnakihitaji na tunaandaa timu kushindana katika msimu huu wa ligi kuu ya Tanzania, kwa PariMatch kwetu mmekuja sehemu sahihi naamini hamtajutia kuwa pamoja na sisi." Amesema Kilua

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad