HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 3, 2022

NIC WATOA ELIMU YA HUDUMA YA BIMA NANE NANE MBEYA



 


Mratibu wa Bima za mazao na Mifugo Prosper Peter (katikati) akimuonyesha kifaa maalum (Ear tags) Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa TIRA Capt. Eliezer Rwekiza (kulia) mara baada ya kufika katika Banda hilo kupata elimu juu ya bima ya Mazao na Mifugo inayotolewa na Shirikaa hilo.
Afisa Bima kutoka NIC Catherine Mjigwa (kushoto) akizungumza jambo na mgeni aliyembelea banda lao katika maonesho ya Nanenane Jijni mbeya.
SHIRIKA la Bima la Taifa (NIC) limeendelea kutoa elimu ya huduma za Bima mbalimbali wanazozitoa katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.

Wananchi wengi wanaotembelea katika Banda la NIC kwenye Maonesho hayo wameonekana wakivutiwa sana na huduma za Shirika hilo ikiwemo Elimu ya Bima hususani ya Mazao ambayo ni bidhaa mpya iliyotokea kuwa msaada na kimbilio kwa wakulima na wafugaji.

Prosper Peter ni Mratibu wa Bima za mazao na Mifugo kutoka Shirika la Bima la Taifa (NIC) anasema kuwa tangu kuanzishwa kwa huduma hiyo kumekuwepo na mwamko mkubwa kwa wadau wa sekta ya Kilimo na Mifugo kujitokeza kujiunga katika Bima hiyo ambapo mpaka sasa kuna zaidi ya wakulima 500 tayari wamejiunga na huduma hiyo.

Kuhusu Mifugo Prosper anasema kuwa, mpaka sasa kuna zaidi ya mifungo 1000 iliyofikiwa na Bima hiyo ambapo katika kuitambua mifugo hiyo kumekuwepo na kifaa maalumu ambayo ni heleni (Ear Tags) anayovalishwa mfugo mmoja hasa kwa Ng'ombe wa nyama na maziwa.

"Kifaa hiki kina usalama sana, mfugo akishavalishwa hakiwezi kutumika kwa mwingine hata kama kitakuwa kimevuliwa, hivyo atatakiwa awe nacho muda wote" anasema Prosper.

Ameitaja mikoa ambayo wafugaji wake wamefikiwa na huduma hii ni pamoja na Mbeya, Tanga na Kilimanjaro, na kwamba NIC inaendelea kuwahamasisha wafugaji katika mikoa mingine kujitokeza kuchangamkia fursa hiyo ili kujihakikishia usalama wa mifugo yao pale wanapopatwa na majanga mbalimbali na kupelekea kifo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad