MWANAMKE AOMBA KUJENGEWA BARABARA ILI AWEZE KUNUNUA GARI “HELA NINAZO” - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 17, 2022

MWANAMKE AOMBA KUJENGEWA BARABARA ILI AWEZE KUNUNUA GARI “HELA NINAZO”

 

Njombe
MWALIMU Betrece Mtweve wa shule ya msingi Ngalawale iliyopo Ludewa kijijini mkoani Njombe ameiomba serikali iwasaidie kujenga barabara katika maeneo yao hususani kuelekea katika shule yao kwa kuwa wamekuwa wakitamani kununua magari kama watu wengine lakini wanashindwa kutokana na kukosa barabara ya kupitisha usafiri.

Mwalimu Betrece amebainisha hilo wakati wa mafunzo ya makarani wa sensa ya watu na makazi walipotembelewa na mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga wilayani hapo ili kuona maendeleo ya mafunzo na kusikiliza changamoto zao.

“Ombi langu kubwa ni barabara,yaani hadi nashindwa kununua gari kwasababu ya barabara mfano kutoka kwenye barabara kuu hadi kuingia shuleni kwangu hususani kipindi cha mvua siwezi kuingia hata kwa pikipiki”amesema Mwalimu Mtweve

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad