MKUU WA MKOA WA RUKWA AVUTIWA NA HUDUMA KWA WANANCHI BANDA LA CHUO KIKUU MZUMBE - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 8, 2022

MKUU WA MKOA WA RUKWA AVUTIWA NA HUDUMA KWA WANANCHI BANDA LA CHUO KIKUU MZUMBE

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa  Queen Sendiga akisaini kitabu cha Wageni katika banda la Chuo Kikuu Mzumbe kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Mwananchi akisaini kitabu cha Wageni katika banda la Chuo Kikuu Mzumbe kwenye maonesho ya kilimo Kitaifa Nane Nane yanayoendelea viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe.Queen Sendiga (kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhadhiri wa Chuo kikuu Mzumbe Ndaki ya  Mbeya Bw.Joshua Mjema wakati alipotembelea banda la Chuo hicho  kwenye maonesho ya kilimo Kitaifa Nane Nane yanayoendelea viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.


MKUU wa Mkoa wa Rukwa Mhe.Queen Sendiga, amewapongeza Watumishi na Menejimenti ya Chuo Kikuu Mzumbe, kwa kuandaa huduma bora wakati wa maonesho ya Kitaifa ya Kiilimo na Mifugo yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Kauli hiyo ameitoa alipotembelea Banda la Chuo Chuo hicho, baada ya kukagua bunifu za wanafunzi na Huduma za ushauri wa kitaalamu zinazotolewa bure kwa wananchi.

Mhe. Queen amesema shughuli zinazoendelea katika Banda hilo, zinawiana na malengo ya maonesho hayo hususani katika kuwaelimisha Wananchi kuhusu ujasiriamali na ushauri wa kisheria, jambo ambalo ndilo msingi wa kukifanya kilimo kuwa ni biashara.

Akimkaribisha Mhe. Queen, Msimamizi wa banda hilo, Bw. Joshua Mjema, amemweleza kuwa, katika maonesho hayo chuo kinatoa huduma mbalimbali zikiwepo bunifu za Wanafunzi wanaozalisha bidhaa ya chai tiba kwa kutumia mbegu za tunda aina ya parachichi, ubunifu wa banda la kufuga na kukuza vifaranga kwa njia ya asili, pamoja na jiko janja linalotumia chenga za mkaa.

Mbali na bunifu hizo, Chuo kinatoa huduma za ushauri bure kwa wananchi, kuhusu masuala ya sheria na biashara, pamoja na elimu ya kujiunga na programu mbalimbali zinatolewa na Chuo na udahili wa papo kwa papo.

Kauli mbiu ya maonesho hayo inasema “Agenda 10/30 Kilimo ni Biashara, shiriki kuhesabiwa kwa Mipango bora ya kilimo mifugo na uvuvi.”

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad