M-BET Tanzania yaidhamini Simba kwa Sh26.1 bilioni kwa miaka mitano - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 1, 2022

M-BET Tanzania yaidhamini Simba kwa Sh26.1 bilioni kwa miaka mitano

 
Na Mwandishi wetu

Dar es Salaam. Kampuni ya mchezo wa kubataisha ya M-Bet Tanzania imeweka historia katika mpira wa miguu hapa nchini baada ya kusaini mkataba mnono wa miaka mitano wenye thamani ya sh Bilion 26.1 klabu ya Simba.

Mkataba huo ni wa kwanza na wa kihistoria kwa hapa Tanzania kwani M-BET inakuwa kampuni ya kwanza kutoa kiasi kikubwa cha fedha hapa nchini kuliko kampuni yoyote.

Mkurugenzi wa Masoko wa M-BET Tanzania, Allen Mushi alisema kuwa mwaka wa kwanza wa mkataba wao, wataipa Simba sh4,670,000,000 ambapo kiasi hicho kitaongezeka msimu wa pili ambapo Simba itapata sh4.9 bilion na mwaka wa tatu wataipa Simba Sh bilioni 5.2

Mushi aliongeza kwa kusema kuwa M-BET itazidi kuiongezea Simba fedha kwani mwaka wanne wataipa Sh5.5 na mwaka wa tano kiasi cha sh5.8 bilioni itapewa Simba.

Alifafanua kuwa wameshawishika na mwenendo na mafanikio mazuri ya klabu ya Simba katika ligi ya nyumbani na mashindano ya kimataifa.

“Hata rangi za Simba zinafanana na sisi. Sisi ni kampuni ya kwanza kuwekeza nchini ambapo mpaka sasa tumetimiza miaka 10 tangu tuanze biashara yetu. Tunajivunia kuwa moja ya kampuni kubwa inayochangia maendeleo ya michezo nchini.

Ni wazi kuwa sisi ni kampuni kubwa na ndiyo maana tumeamua kushughulika na klabu kubwa Tanzania pamoja na Afrika, huu ni mkataba wa kihistoria na tunatarajia kuendelea na mkataba mwingine mara baada ya mkataba huu kumalizika,” alisema Mushi.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez aliishukuru M-BET Tanzania kwa kukubaliana na masharti yao mpaka kusaini mkataba wenye thamani kubwa hapa nchini.

"Tulianza mazungumzo na M-BET Tanzania miezi michache iliyopita na hatimaye tukapata kile tulichokuwa tunakitaka. Ni hatua kubwa sana kwa klabu. Tutaonyesha dhamira yetu kwa wadhamini wetu ili kufanya mkataba huo uwe na nguvu zaidi," alisema Barbara.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa M-BET nchini, Fernando Perez akisema kuwa mkataba huo unaonyesha nia ya kampuni yao ya kuleta maendeleoya dhati hapa nchini.

"Ni siku ya kipekee sana kwa M-BET Tanzania na kwangu kama Meneja wa M-BET Tanzania hapa nchini. Nimefurahi sana kufanikisha mkataba huu wenye kuleta tija kwa Simba na kuchangia maendeleo ya mpira hapa nchini," Perez alisema.Maofisa wa kampuni ya namba moja ya michezo ya kubashiri nchini, M-BET Tanzania na viongozi wa Simba katika picha mbalimbali za utambulisho rasmi wa mkataba wa miaka mitano baina ya pande hizo mbili. Mkataba huo utaigharimu M-BET Tanzania kuwapa Simba Sjh 26.1 billion kwa kipindi cha miaka mitano.
No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad