HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, August 28, 2022

Baadhi ya wateja wakifurahia bidhaa ya Yogurt inayozalishwa na mfanyabiashara Lulu Yasin katika maonesho hayo yaliyowakutanisha wafanyabiashara kutoka Tabata na maeneo mengine ya Jiji la Dar es Salaam.
 
Doreen Frowin (kushoto,) ambaye ni mfanyabiashara wa nguo za kike akimuhudumia mmoja nya wateja aliyekuja kupata huduma katika maonesho hayo ya Tabata Pop Up yaliyofanyika katika viwanja vya Nyantare Tabata jijini Dar es Salaam.



WAFANYABIASHARA kutoka Tabata na maeneo mengine ya jiji la Dar es Salaam wamekutana kupitia maonesho ya biashara ya ‘Tabata Pop Up’ na kupata fursa ya kutangaza bidhaa pamoja na kubadilishana uzoefu ili kujijenga vizuri kibiashara.

Akizungumza katika maonesho hayo mjasiriamali Debora Mavura ambaye ni  muandaaji wa Tabata Pop Up lakini pia mzalishaji na muuuzaji bidhaa za Dekit Slippers (Malapa ya kutembelea ndani) amesema maonesho hayo ya biashara yamefanyika kwa  lengo la kuwakutanisha wafanyabiashara na kupata fursa ya kutangaza bidhaa zao pamoja na kubadilishana ujuzi na uzoefu ili kujijenga zaidi kibiashara na kupata fursa za masoko.

Bi. Debora amesema kukutana kwa wafanyabiashara  hao kutasaidia kutangaza  na kuonesha bidhaa zao katika soko la Tabata na maeneo mengine pamoja na kubadilishana mawazo ya kukuza zaidi biashara zao.

‘’Soko la Tabata ni kubwa, kuna vitu na watu wengi. Kwa kipindi kifupi sana jina la tabata limekua Kwa Kasi kubwa, hii ni Moja ya sababu iliyomfanya bi. Debora kuona fursa chanya na kuitumia Ili kuweza kuonesha jamii ya tabata na nje ya tabata vitu vizuri na vya maendeleo vinavyoweza patikana tabata, ikiwemo hivi tunavyoonesha leo. Tabata Kuna fursa  mbalimbali na kwa kupitia vijana kutoka hapa Tabata na maeneo mengine tutaendelea kuhamasishana katika kushiriki katika maonesho haya ya kutangaza bidhaa ili kuweza  kujijenga zaidi katika biashara na masoko kwa ujumla.’’Amesema.

Bi. Deborah amesema amekuwa akishiriki maonesho mbalimbali ya ujasiriamali na kuzichukua changamoto kama fursa ambazo kwa kukutana na wajasiriamali hao watapeana elimu na mwelekeo wa kuboresha biashara zao.

Aidha amesema kuwa wataendelea kukutana kupitia maonesho ya namna hiyo ili kupata nafasi ya kujitangaza pamoja na kujikuza kibiashara na kuweza kuwainua vijana wengine.

Maonesho hayo yamehusisha washiriki kumi waliopata fursa ya kutangaza bidhaa mbalimbali ikiwemo mavazi, bidhaa za ngozi, vipodozi pamoja na vinywaji.

Baadhi ya washiriki wa maonesho hayo wameshukuru kwa ushirikishwaji katika maonesho hayo ya Tabata Pop Up na kuomba uendelevu wa maonesho ya namna hiyo ambayo husaidia zaidi katika kutangaza bidhaa zao na kupata masoko.

Maonesho yakiendelea.
Mfanyabiashara wa bidhaa za urembo Glory Kimaro (kulia,) akimuhudumia mteja aliyekuja kupata huduma katika maonesho hayo ya kutangaza bidhaa yaliyowakutanisha wafanyabiashara kutoka Tabata na maeneo mengine ya Jiji la Dar es Salaam.
Muonekano wa baadhi ya bidhaa.
Mfanyabiashara wa nguo na bidhaa za kike Nice Magesa (kushoto,) akibadilisha mawazo na Doreen Frowin ambaye ni mfanyabishara wa nguo za kike katika maonesho ya kutangaza bidhaa yaliyowakutanisha na kufanyika katika viwanja vya Nyantare Tabata jijini Dar es Salaam.
Muandaaji wa maonesho hayo Debora Mavura (kushoto,) akiwa na mmoja ya washiriki wa maonesho hayo ya kutangaza bidhaa maarufu kama Tabata Pop Up yaliyofanyika katika viwanja vya Nyatare jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa bidhaa za ngozi zinazozalishwa na kusambazwa na kampuni ya AMIMETA VENTURES LTD ya jijini Dar es Salaam.
Mfanyabishara wa bidhaa za ngozi kutoka kampuni ya AMIMETA VENTURES LTD Adam Niyonzima akiwa katika maonesho hayo ya kutangaza bidhaa yaliyowakutanisha wafanyabiashara kutoka Tabata na maeneo mengine ya Jiji la Dar es Salaam.
Mfanyabiashara wa vifaa vya umeme Prince Enock akipanga bidhaa wakati wa maonesho ya kutangaza bidhaa 'Tabata Pop Up' yaliyowakutanisha wafanyabiashara kutoka Tabata na maeneo mengine ya Jiji la Dar es Salaam.
Maonesho ya bidhaa yakiendelea.
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad