HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, July 7, 2022

WAZIRI NAPE AZITAKA TAASISI ZA SERIKALI KUTUMIA ‘VIDEO CONFERENCE’ KUPUNGUZA GHARAMA

 Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye akizungumza na jambo na watumishi wa TTCL wa Jijini Dodoma kwa njia ya 'Video Conference' akiwa ndani ya Banda la TTCL kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) ndani ya Banda la TTCL kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Mhandisi Peter Ulanga.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye akizungumza na watumishi wa TTCL wa Jijini Dodoma kwa njia ya 'Video Conference' akiwa ndani ya Banda la TTCL kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Biashara wa TTCL, BW. Vedastus Mwita akifafanua jambo kwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye kuhusiana na huduma ya Faiba Mlangoni Kwako ndani ya Banda la TTCL.


Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Mhandisi Peter Ulanga akifafanua jambo kwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye kuhusiana na huduma ya Faiba Mlangoni Kwako ndani ya Banda la TTCL.


Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Mhandisi Peter Ulanga (kulia) akimkabidhi zawadi Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye kwa ishara ya kumshukuru kwa kutembelea Banda la TTCL kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye akipata maelezo juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na TTCL ndani ya Banda la TTCL kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.


WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe Nape Nnauye ametembelea banda la Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara na kuziagiza taasisi za Serikali kutumia teknolojia ya TEHAMA ya 'video conference' kwenye mikutano yao.

Waziri Nnauye amesema matumizi hayo ya TEHAMA yatasaidia kiasi kikubwa kupunguza gharama za Serikali huku hatua hiyo pia ikirahisisha mawasiliano kwa shughuli za Serikali na watumishi wake.

Mhe. Nnauye amebainisha hayo alipotembelea Banda la Shirika la TTCL kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Akiwa katika Banda la TTCL amepata fursa ya kuona huduma mbalimbali zinazotolewa na TTCL ikiwemo huduma ya Faiba Mlangoni Kwako, iliyowavutia zaidi wadau wa mawasiliano nchini.

Ameonesha pia kuvutiwa na huduma ya Video Mtandao na kulipongeza Shirika hilo kwa hatua madhubuti zinazochukuliwa katika kuhakikisha huduma hiyo inaunganishwa katika ofisi za Serikali na taasisi zake.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Mhandisi Peter Ulanga akizungumza na vyombo vya habari shirika hilo limejipanga kuhakikisha linaziunganisha taasisi na ofisi za Serikali katika matumizi ya TEHAMA ili kurahisisha shughuli zote za Serikali ikiwemo mikutano.

Amesema TTCL ndiyo mtoa huduma wa kwanza kutekeleza agizo la Serikali la kutumia 'video comference' katika mikutano yake na kwamba lengo la Serikali kutaka kutumia huduma hii ni kupunguza gharama na kuwakutanisha watumishi kwa njia ya haraka zaidi.

Amesema mpaka sasa TTCL imeshawaunganisha wateja zaidi ya 10 mkoani Dodoma ambao wanaendelea kufurahia huduma baada ya kufungiwa mfumo huo.

Akizungumzia huduma Faiba Mlangoni, Mhandisi Ulanga amebainisha kuwa huduma hiyo ina umuhimu mkubwa kwa mteja kwani itamwongezea uwezo wa kutumia intaneti kwa haraka na ubora zaidi hivyo kuwashauri wateja kuitumia ili kufurahia mawasiliano rahisi.

Ameongeza kuwa huduma ya Faiba Mlangoni inaingia Sokoni kwa lengo la kubadili soko zima la matumizi ya TEHAMA kwa kuboresha zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad