WATENDAJI WA HALMASHAURI MIKOA YA KANDA YA KASKAZINI WANOLEWA JUU YA SHERIA ZA MBEGU - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 13, 2022

WATENDAJI WA HALMASHAURI MIKOA YA KANDA YA KASKAZINI WANOLEWA JUU YA SHERIA ZA MBEGU

 Maafisa kilimo, mipango na wanasheria wa halmashauri za mikoa ya kanda ya kaskazini mwa Tanzania wameelezwa mabadiliko ya sheria za mbegu na wameombwa wazingatie mabadiliko hayo wanapoandaa sheria ndogo katika halmashauri zao ili usiwepo utata wa matumizi wa sheria hizo nchini.


Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua semina elekezi juu ya suala hili jijini hapa jana, Meneja wa Sera wa Kituo cha Kuendeleza Kilimo Nyada za Juu Kusini mwa Tanzania (Sagcot), Bw.Khalid Mgalamo, alisema lengo la semina hiyo nikuwajengea uwezo watendaji wa halmashauri juu ya mabadiliko yaliyofanyika katika ngazi ya tiafa ili sheria ndogo wanapoziandaa zisitofautiane au kukinzania na mabadiliko yaliyopo ngazi ya taifa.

Semina hiyo ya siku moja imeandaliwa na Sagcot ikishirikiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), kwa ufadhili wa Agra imehudhuriwa na maafisa 80 kutoka halmashauri 20 za mikoa ya kanda ya kaskazini ikiwemo Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Morogoro

Bw Mgalamo alisema: “Semina hii imefanyika kwa mikoa ambayo inamazingira wezeshi ya uzalishaji wa mbegu na nia yetu ni kuwajengea uelewa wa mabadiliko ya sheria za mbegu na tozo mbalimbali yaliyofanyika katika ngazi ya taifa ili sekta ndogo ya mbegu iendelee kuimarika.”

Alieleza wambia wanasemina hao kuwa tozo za mbegu zilizowekwa na halmashauri zote imeondolewa katika mwaka huu wa fedha wa 2022/23 na kusisitiza kwamba jambo hilo lifahamike katika ngazi zote ili kuondoa mgongano kati watendaji wa halmashauri na wazalishaji wa mbegu.

“Kupitia semina hii tunatoa ujumbe kwamba uaandaji wa sheria ndogo katika halmashauri lazima uzingatie maboresho ya sheria na sera yaliyofanyika katika ngazi ya taifa jambo litakalosaidia kuongezeka kwa uzalishaji wa mbegu nchini,” alisema Bw.Mgalamo

Mkuu wa Uratibu wa Sekta za Uchumi na Uzalishaji wa Tamisemi, Bw.Leo Mavika, alisema semina hii imekuja wakati muafaka kwani kuna mabadiliko mengi ya sheria ngazi ya taifa kuhusu tozo na kodi mbalimbali hususani za mbegu, hivyo semina hii itasaidia sana kuwajengea uelewa watendaji juu ya mabadiliko hayo.

“Ofisi ya Rais Tamisemi ndio watekelezaji wa sheria, sera, miongozo na kanuni mbalimbali. Hivyo semina hii imekuwa ni sehemu nzuri ya kukumbushana na kujengeana uelewa wapamoja juu ya mabadiliko mbalimbali ya sheria yanayoendelea kufanyika. Lengo ni kuboresha mazingira ya kufanya uzalishaji wa mbegu na usimamizi na utungaji mzuri wa sheria ndogo,” alisema Bw.Mavika

Afisa Miradi wa Shirika la Mapinduzi ya Kijani Afrika(AGRA), Bw.Ipyana Mwakasaka, alisema semina hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa kuboresha sheria na sera za mbegu ili kuongeza uzalishaji wa mbegu ili Tanzania iweze kujitegemea kwa mbegu na hata kuuza mbegu nje na kuahidi kwamba taasisi yao itaendelea kushirikiana na serikali katika kuboresha sekta ndogo ya mbegu na kuhakikisha mkulima anapata mbege kwa gharama nafuu.

“AGRA itaendelea kushirikiana na Serikali na wadau wengine katika sekta ya kilimo ili kuhakikisha sekta ndogo ya mbegu inaboreshwa kwa kuzalishaji mbegu bora na mbegu kumfikia mkulima kwa gharama nafuu jambo litakaloongeza uzalishaji wa mazao nchini,” alisema Bw.Mwakasaka
Mkuu wa Kitengo cha Majaribio ya Umahiri kutoka Taasisi ya kuthibiti ubora wa mbegu Tanzania(TOSCI) Dkt.Adolf Saria akitoa maelezo juu ya mabadiliko mablimbali yaliyofanyika kuhusu mbegu kwa maafisa kilimo, mipango na wanasheria wa halmashauri za mikoa ya kanda ya kaskizini katika semina elekezi juu ya mabadiliko ya sheria na namna ya uandaa wa sheria ndogo katika halmashauri zao ziendane na sheria za taifa.
Meneja wa Sera wa Kituo cha Kuendeleza Kilimo nyanda za juu kusini mwa Tanzania (SAGCOT) Bw.Khalid Mgalamo akitoa maelezo juu ya mabadiliko mablimbali yaliyofanyika kuhusu mbegu kwa maafisa kilimo, mipango na wanasheria wa halmashauri za mikoa ya kanda ya kaskizini katika semina elekezi juu ya mabadiliko ya sheria na namna ya uandaa wa sheria ndogo katika halmashauri zao ziendane na sheria za taifa.
Meneja wa Sera wa Kituo cha Kuendeleza Kilimo nyanda za juu kusini mwa Tanzania (SAGCOT) Bw.Khalid Mgalamo(kulia) akizungumza jambo na Mkuu wa uratibu wa sekta za uchumi na uzalishaji wa TAMISEMI, Bw.Leo Mavika(kushoto) katika semina elekezi juu ya mabadiliko ya sheria na namna ya uandaa wa sheria ndogo katika halmashauri kwa maafisa kilimo, mipango na wanasheria wa halmashauri za mikoa ya kanda ya kaskizini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad