HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 5, 2022

WANANCHI WAKARIBISHWA BANDA LA TIC

Kaimu Mkurugenzi Idara ya uhamasishaji Uwekezaji katika Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Levocatus Rasheli akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika maoneosho ya kimataifa ya kibiashara yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wafanyakazi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) wakiwa katika picha ya pamoja.
Mfanyakazi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) akizungumza na wananchi walipotembelea maonesho ya Sabasaba jijini Dar Es Salaam.
Hapa nchi Kriniki ya biashara katika maonesho ya Kimataifa ya biashara ya 46 yanayofanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar Es Salaam.

IKIWA Serikali ipo katika utekelezaji wa mradi wa mpango wa tatu wa maendeleo wa mwaka 2020, 2021 hadi 2025, 2026 kituo cha uwekezaji Tanzania kimewakaribisha watanzania kwenye banda la TIC, lililopo katika maonesho ya kimataifa ya kibiashara 46 jijini Dar Es Salaam kujipatia elimu na jinsi ya kuwekeza nchini.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya uhamasishaji Uwekezaji katika Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Levocatus Rasheli amewakaribisha watanzania katika maonesho hayo ya sabasaba ili kufanya usajili na kupata cheti cha uwekezaji nchini.

"Nichukue fursa hii kuwakaribisha watanzania wote, lakini pia wawekezaji wote na wafanyabiashara wote waweze kupita katika maeneo haya ili muweze kuongea na watoa huduma wetu pamoja na kupata taarifa kuhusu masuala ya kuhamasisha, kuhudumia na kufanikisha uwekezaji hapa nchini." Amesema Rasheli

Amesema TIC imeweka mabanda katika maeneo matatu kweny maonesho hayo ili watembeleaji wanapopita katika maeneo hayo waweze kupata majarida na vipeperushi mbalimbali kwaajili ya kujipatia elimu juu ya uwekezaji. Lakini pia amesema kuwa unaweza kupata elimu hiyo kieletroniki na kwa njia yamajarida ili wawekezaji waweze kupata taarifa kiurahisi na kufanya maamuzi ya uwekezaji.

Amesema kuwa serikali imeweka nguvu zaidi katika mpango wa maendeleo katika maeneo ambayo watanzania wanazalisha bidhaa mbalimbali hasa bidhaa za kilimo, bizaa zinazotokana na misitu, bidhaa za uvuvi na maligafi kwaajili ya Ufugaji pamoja na Maligafi zinazotumika katika uchimbaji madini.

Amesema kuwa nia ya Serikali ni kuhakikisha wanapata masoko wazalishaji wa malighafi zaidi ya asilimia 70 waliopo nchini.

Amesema masoko hayo ni kuwa na viwanda nchini, ambapo viwanda hivyo Vitachukua maligafi hizo na kupeleka viwandani kwaajili ya kuzitengezea thamani na kuzalisha bidhaa za mwisho kwaajili ya mtumiaji.

"Hapa tunazalisha ajira mpya za wazalisha malighafi, ajira za viwandani lakini pia tunaongeza thamani kwa kuzipeleka bidhaa kwenye masoko ndani na nje ya nchi, hapo tunakuwa tumeongeza pato la taifa." Amesema Rasheli

Amesema kuwa katika mabanda ya TIC wanatoa taarifa juu ya wawekezaji wa ndani pamoja na wawekezaji wa nje. Taratibu zote zimewekwa ili kila anayetembelea apate taarifa anayostahili wakishapata taarifa wanapata maamuzi ya kufanya uwekezaji." Amesema

Rasheli amesema kuwa Watanzania wenye mali mbalimbali zinazopelekea kuwa na uwekezaji wanauwezo wa kupeleka taarifa hizo ili waweze kuwekeza.

Amesema wameshapata taarifa za watu wenye ardhi katika maeneo ya kimkakati, pia wenye ardhi maeneo kama hayo watoe taarifa ili waweze kuwaunganisha na wawekezaji.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad