TANZANIA YASIFIWA INAFANYA VIZURI KATIKA CHANJO ZA UVIKO-19 - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 6, 2022

TANZANIA YASIFIWA INAFANYA VIZURI KATIKA CHANJO ZA UVIKO-19

 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amekutana na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeratibu msauala ya UVIKO-19, Dkt. Ted Chaibans jijini Dar Es Salaam tarehe 5 Julai 2022.

Katika kikao hicho, Balozi Mulamula alielezea hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania za kudhibiti ugonjwa wa UVIKO-19 na kusisitiza umuhimu wa Jumuiya ya Kimataifa kuendelea kushirikiana na Tanzania kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Balozi Mulamula alisema licha ya changamoto za uhaba wa miundombinu na ukubwa wa nchi, Serikali imejitahidi kupambana na ugonjwa huo, hususan kwa kuhamasisha wananchi wajitokeze kupata chanjo za UVIKO-19.

Balozi Mulamula alihitimisha mazungumzo hayo kwa kukumbushia wito wa Serikali kuhusu kupata msaada wa Jumuiya ya Kimataifa ili Serikali ya Tanzania iweze kutimiza azma yake ya kujenga kiwanda cha kutengeneza chanjo za Uviko-19 na magonjwa mengine.

Kwa upande wake, Dkt. Chaibans alikiri kuwa licha ya Tanzania kuchelewa kuanza matumizi ya chanjo za UVIKO-19 lakini imepiga hatua kubwa kuliko baadhi ya nchi zilizoanza mapema kampeni za kuhamasisha chanjo. Alisisitiza umuhimu wa Serikali kuendelea kuhamasisha watu kwa kubuni mbinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwatumia viongozi wa dini. Aliendelea kwa kutoa wito kwa Serikali ya Tanzania, ihakikishe kuwa makundi ya kipaumbele kama Wazee, wenye maradhi ya kudumu, watumishi wa sekta za afya, elimu na utalii wanahamasishwa ili wapate chanjo za UVIKO-19.

Wakati huo huo, Balozi Mulamula amekutana na wajumbe wa Kamati ya Afrika ya Hydrogen inayojihusisha na uwekezaji katika nishati jadidifu (renewable energy). Wajumbe wa Kamati hiyo walimweleza Mhe. Waziri Mulamula utajiri wa vyanzo mbalimbali vya nishati ilivyonavyo Tanzania ambavyo vina fursa nyingi za kibiashara, endapo vitatumiwa vizuri. Kamati hiyo imeelezea utayari wa kufanya kazi na Serikali ya Tanzania kuhakikisha kuwa rasimali hizo zinatumika vizuri ili ziweze kuleta maendeleo endelevu.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimkaribisha Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeratibu masuala ya UVIKO-19, Dkt. Ted Chaiban ili waweze kujadili masuala ya UVIKO-19.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiongea na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeratibu masuala ya UVIKO-19, Dkt. Ted Chaiban ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi.
Ujumbe ulioambatana na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeratibu masuala ya UVIKO-19, Dkt. Ted Chaiban ukifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeratibu masuala ya UVIKO-19, Dkt. Ted Chaiban.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeratibu masuala ya UVIKO-19, Dkt. Ted Chaiban wakiendelea na mazungumzo yao huku ujumbe wa Tanzania ukifuatilia kwa makini mazungumzo hayo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeratibu masuala ya UVIKO-19, Dkt. Ted Chaiban wakisikiliza ufafanuzi wa jambo kutoka kwa mtaalamu wa UN kuhusu UVIKO-19.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiteta jambo na mmoja wa mjumbe aliyeambatana na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeratibu masuala ya UVIKO-19, Dkt. Ted Chaiban.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeratibu masuala ya UVIKO-19, Dkt. Ted Chaiban wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe walioambatana nao wakati wa mazungumzo kuhusu UVIKO-19.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Kamati ya Afrika ya Hydrogen ambayo inajishughulisha na masuala ya kutoa ushauri na uwekezaji katika Nishati jadidifu (renewable energy).
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika picha y pamoja na wajumbe wa kamati ya Afrika ya Hydrogen.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad