HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 12, 2022

SERIKALI YAAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO NA KAMPUNI YA UNILEVER

 


KATIBU Tawala Uchumi na Uzalishaji wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk Elizabeth Mshote ameipongeza Kampuni ya Unilever ambayo ni watengenezaji wa Sabuni ya Omo kwa namna ambavyo wamekua mstari wa mbele katika kushirikiana na Serikali katika mambo ya kijamii.

Mshote ametoa pongezi hizo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa muonekano mpya wa Sabuni ya Omo iliyoboreshwa zaidi ambapo amesema Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za wawekezaji wanaokuja kuwekeza nchini.

Dk Mshote amesema Kampuni ya Unilever kupitia bidhaa yake ya Omo wamekua wadau wakubwa wa Serikali na Watanzania kwa ujumla na kwamba anafarijika kuona wakizindua muonekano mpya wa Sabuni hiyo.

" Wote tunatambua ya kwamba Unilever ni kampuni kubwa na ya kimataifa ambayo bidhaa zake wengi wetu humu hutumia kila siku. Kuna sabuni ambazo kila siku tunatumia kwenye kufua, mafuta ambayo kila siku tunajipaka na royco ambayo ukitaka mboga iwe tamu lazima tutumie.

Bidhaa za Unilever ni bidhaa zenye ubora wa hali ya juu na zimekidhi vigezo vyote vya kimataifa. Ninayo furaha kushiriki kwenye uzinduzi huu wa muonekano mpya wa sabuni ya Omo iliyoboreshwa zaidi," Amesema Dk Mshote.

Amesema Unilever Tanzania na Sabuni yao ya Omo wamekuwa Mstari wa Mbele katika kushiriki mambo ya Kijamii katika mkoa wetu wa Dar es salaam hususani katika kutoa Msaada wa Shuka Pamoja na sabuni kwenye Hospital zifuatazo Muhimbili Hospitali, Mwananyamala Hospitali na Amana Hospitali.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Unilever Tanzania, David Ninja amemshukuru Katibu Tawala Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Dar es Salaam, Dk Elizabeth Mshote kwa kufika kushiriki tukio hilo la uzinduzi wa muonekano mpya wa Sabuni ya Omo ambapo pia amewahakikishia watanzania kwamba ubora wa bidhaa hiyo umeongezeka maradufu.

" Kampuni ya Unilever imekuwa ikienda sambamba na ukuaji wa teknolojia duniani ili kuendana na hali ya soko na hususani kwa wateja wake.

hivyo leo ni siku muhimu sana kwetu kwani tunazindua muonekano mpya wa sabuni ya Omo iliyoboreshwa zaidi kwa lengo la kuendelea kuvutia watumiaji wa sabuni hii.

Naomba nichukue fursa hii kuwaambia wateja wetu na jamii ya Kitanzania kwamba ujumbe wetu kwa leo ni kuwa OMO NI MKALI WA MADOA SUGU ni sabuni namba moja kwa kuondoa madoa sugu na kwa haraka zaidi kwani unga na vimeng’enya viliyomo ndani mwake ni mzuri na huondoa uchafu kwa haraka Zaidi na kuacha nguo yako ikiwa na harufu nzuri (manukato) ndani ya siku 14," Amesema Minja.

Amesema Kampuni ya Unilever kwa kupitia sabuni yake ya Omo imekuwa mstari wa mbele katika kurudisha kile kidogo tupatacho kwa watanzania na kuungana na watanzania katika kujenga Maisha bora kwa wote.

" Tumekuwa na kampeni mbalimbali kama MKONO WA SHUKRANI, kwa mwaka jana, kampeni hii ilifanyika katika Hospitali tatu jijini Dar es salaam Muhimbili, Mwananyamala Pamoja na Hospitali ya Amana, ambapo tulichangia mashuka Pamoja na sabuni kwa ajili ya watanzania wenzetu, Pia Omo tumekuwa na kampeni ya Mkono Wa Ukarimu, kampeni maalum kabisa wakati wa kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kampeni hii ilifanyika na tulikusanya nguo kutoka kwa watanzania wenzetu na tukafua kwa kutumia Omo na pia tukaenda kuzikabidhi kwa wale watu wenye uhitaji," Amesema.

 


Pichani kushoto ni Mgeni rasmi Katibu Tawala wa Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Dar es Salaam Dkt Elizabeth Mshote pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Unilever Tanzania, David Minja kwa pamoja wakizindua muonekano mpya wa sabuni ya OMO iliyoboreshwa zaidi kwenye hafla fupi iliofanyika jana jijini Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-MMG.



Mgeni rasmi Katibu Tawala wa Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Dar es Salaam Dkt Elizabeth Mshote akizungumza mbele ya Wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla ya uzinduzi wa muonekano mpya wa sabuni ya OMO iliyoboreshwa zaidi uliofanyika jana jijini Dar es Salaam



Mkurugenzi Mtendaji wa Unilever Tanzania, David Minja akizungumza mbele ya Wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla ya uzinduzi wa muonekano mpya wa sabuni ya OMO iliyoboreshwa zaidi uliofanyika jana jijini Dar es Salaam


Sehemu ya Meza kuu akifuatilia yaliyokuwa yakijiri wakati wa uzinduzi wa muonekano mpya wa sabuni ya OMO iliyoboreshwa zaidi

Meneja Masoko kampuni ya Unilever Tanzania,Upendo Mkusa akizungumza mbele ya Wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla ya uzinduzi wa muonekano mpya wa sabuni ya OMO iliyoboreshwa zaidi jana jijini Dar es Salaam
Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi huo kufanyika
Msanii wa muziki wa kizazi kipya (singeli) atambulikae kwa jina la kisanii Shalo Mwamba akitumbuiza wageni waalikwa kwenye hafla hiyo
Mkurugenzi Mtendaji wa Unilever Tanzania, David Minja akijiachia pamoja na msanii Shalo Mwamba katika vionjo vya miondoko ya Singeli


Shalo Mwamba akitumbuiza kwenye hafla hiyo






Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad