SEKTA BINAFSI WAASWA KUCHANGAMKIA FURSA SEKTA YA GESI ASILIA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 8, 2022

SEKTA BINAFSI WAASWA KUCHANGAMKIA FURSA SEKTA YA GESI ASILIA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) Dkt.James Matarangio akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea Banda la TPDC Katika Maonesho ya Kimataifa ya kibiashara ya 46 yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya J.K.Nyerere Maarufu kama Sabasaba jijini Dar Es Salaam leo Julai 7, 2022. 

WAWEKEZAJI kutoka Sekta binafsi wameaswa kuchangamkia fursa ya ujenzi wa Vituo Vidogo vidogo vya kusambaza vya gesi asilia nchini.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) Dkt.James Matarangio wakati akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea Banda la TPDC Katika Maonesho ya Kimataifa ya kibiashara ya 46 yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya J.K.Nyerere Maarufu kama Sabasaba jijini Dar Es Salaam leo Julai 7, 2022. Amewahamasisha Sekta Binafsi kwenda TPDC kupata idhini ya kujenga vituo hivyo.

"Rai yanga kwa sekta binafsi wajitokeze kwa wingi ili kushiriki kujenga vituo vidogo vidogo na hizo ndio fursa katika sekta ya Nishati ya Gesi asilia hapa nchini." Amesema Dkt. Matarangio

"Na mpaka sasa tunamradi wa kujenga vituo vitano vya SMG vinajengwa Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam, Feri, Muhimbili, Kibaha na Kituo cha Mabasi cha Ubungo (zamani) vituo hivyo vitakamilika mwakani Machi 2023." Amefafanua Dkt. Matarangio.

Amesema kuwa ujio wa Vituo Vitano vya Gesi asilia vitaambatana na ujio wa vituo vingine vidogo vidogo katika maeneo mbalimbali hapa nchini kwasababu gesi ikiwekwa kwenye mitungi inaweza kusafirishwa popote.

Amesema kuwa Kiasi cha gesi ambacho kimekigundulika baharini mpaka sasa ni futi za ujazo trilioni 57. 54 gesi hiyo inatarajiwa kuvunwa.

Dkt. Matarangio amesema Matumizi makubwa ya gesi hapa nchini asilimia 62 ya umeme wa Tanzania unatokana na gesi asili na kiasi kinachobakia cha gesi cha asilimia 20 kinachozalishwa kinatumika majumbani na kwenye magari.

"Ili kukivuna kiasi hicho kilichopo baharini tunajenga mtambo wa kusindika gesi asilia na kuwa kimiminika (LNG), mitambo hii itachakata ile gesi inayovunwa baharini, inapoozwa mpaka ubaridi wa nyuzi joto hasi 160 na kusafirishwa kwenda kuuzwa kwenye masoko." Amesema Dkt. Matarangio

Amesema kuwa Kiasi cha fulani cha gesi hiyo kitabaki nchini kwaaajili ya soko la ndani na soko la Afrika Mashariki hasa Uganda Kenya na Zambia.

Kuhusiana na Mradi wa LNG amesema kuwa Katika majadiliano ya mradi wa wa kusindika gesi asilia na kuwa kimiminika (LNG) makubaliano ya awali yalifanyika na kusainiwa Juni, 2022 Ikulu ya Chamwino mbele ya Rais, Samia Suluhu Hassan.

Amesema lengo ifikapo Desemba wawewameshakubaliana na kunasaini Mkataba hodhi wa nchi.Baada ya kusaini makubaliano ya mkataba hodhi wa Taifa watanza kuingi katika hatua nyingine ya kiuhandisi na kuanza kupanga mipango ya kujenga Kiwanda.
kwa upande wa Mkondo wa chini ambao ni Usambazaji Dkt. Matarangio amesema kuwa watajenga miundombinu ya kusambaza Gesi majumbani, kwenye vyuo na kwenye magari.

Amesema kuwa Watanzania mpaka sasa wanafaidi matunda ya gesi lakini TPDC wanahitaji kuongeza zaidi ili kuhakikisha watumiaji wa magari yanayotumia gesi asilia wanafaidika kwa kutumia gesi, wananchi wanafaidika kwa kutumia gesi.

Amesema gesi inayotarajiwa kuivunwa kutoka baharini wanataka itumike sio tuu kuzalisha umeme lakini itumike kama marigafi ya kutengeneza bidhaa mfano bidhaa za plastiki.

"Gesi itatumika kutengeneza bidhaa zote za plastiki na mbolea na tunampango wa kujenga Viwanda vya Mbole na Plastiki ili kukuza pato la taifa.

"Ile gesi itayoenda kuuzwa nje ya nchi tunatarajia serikali itapata mapato makubwa na fedha za kigeni."

Amesema Matumizi ya gesi asilia yanafaida kwasababu ni safi, rafiki wa mazingira kwahiyo matumizi ya gesi asilia yatapunguza uchafuzi wa mazingira.

"Kama watu wote wakiweza kutumia gesi basi tutatunza miti yetu vizazi vijavyo viweze kuwa na mazingira mazuri."

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad