HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 26, 2022

RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK.HUSSEIN MWINYI AMEWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA SKULI YA MSINGI MAKANGALE PEMBA

 


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiondoa pazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Skuli ya Msingi ya Makangale Wilaya ya Micheweni Pemba, inayojengwa kwa Fedha za Uviko-19, na (kushoto kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi, hafla hiyo ya uwekaji wa Jiwe la Msingi iliyofanyika leo 26-7-2022.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi, akisoma maelezo ya Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Skuli ya Msingi Makangale Pemba, ninayojengwa kwa Fedha za Uviko-19, wakati wa ziara yake kutembelea Miradi ya Maendeleo katika Mikoa Miwili ya Pemba.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mhandisi wa Kampuni ya Ujenzi ya Masasi Const Ndg. Mathias John Msila akitowa maelezo ya michero ya jengo la Skuli ya Msingi Makangale, wakati wa hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi huo leo 26-7-2022, linalojengwa kupitia Fedha za Uviko-19.na (kulia kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.Mhe Lela Mohammed Mussa na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe.Salama Mbarouk.(Picha na Ikulu)
MUONEKANO wa Jengo Jipya la Skuli ya Msingi Makangale Wilaya ya Micheweni Pemba, lililowekwa Jiwe la Msingi la Ujenzi huo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, linalojengwa kwa Fedha za Uviko -19.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, akizungumza na kutowa maelekezo kwa Uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, wakati akitembelea moja ya madarasa katika jengo hilo la Skuli ya Msingi Makangale baada ya kuweka jiwe la msingi, (kushoto kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Mohammed Mussa. Skuli hiyo inayojengwa kwa Fedha za Uviko-19.(Picha na Ikulu)


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad