RAIS MWINYI AFANYA ZIARA MKOA WA MJINI MAGHARIBI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, July 17, 2022

RAIS MWINYI AFANYA ZIARA MKOA WA MJINI MAGHARIBI

 


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi  wakati alipowasili viwanja vya ukumbi wa Chuo cha Utalii Maruhubi  Wilaya ya Magharibi”A” wakati akianza ziara yake ya  kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo.[Picha na Ikulu] 16/07/2022.
Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Mapinduzi na  Serikali wakiwa katika  hafla ya usomwaji wa Ratiba ya ziara ya Rais wa Zanziar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi aliyoianza leo kwa kutembelea miradi ya maendeleo katika maeneo ya Shehia mbali mbali  za Wilaya ya Magharibi”A”huko katika ukumbi wa Chuo cha Utalii Maruhubi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi alipokuwa akisoma kitabu cha ratiba  iliyokuwa ikisomwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi  Mhe.Idrissa Kitwana Mustafa (hayupi pichani) katika ukumbi  wa Chuo cha Utalii  Maruhubi leo kabla ya kuanza ziara katika Wilaya ya Magharibi”A” ya kutemelea na kuangalia miradi mbali mbali ya maendeleo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi alipokuwa akimsikiliza Mkuu wa Jeshi la kujenga Uchumi JKU Kanali Makame Abdalla Daima kuhusu Ujenzi wa Skuli ya Kihinani Msingi iliyojengwa na Kikosi chake  Ujenzi wa madarasa kumi  na mbili kupitia fedha za UVIKO  19, wakati wa  ziara ya   kutembelea na kuangalia miradi mbali mbali ya maendeleo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (wanne kulia)alipokuwa akisoma maandishi ya jiwe la msingi Hospitali ya Wilaya Mbuzini mara ya kufungua pazia jiwe hilo ikiwa ni ishara ya ufunguzi rasmi wa Hospitali hiyo leo akiwa katika  ziara ya   kutemelea na kuangalia miradi mbali mbali ya maendeleo kwa Wilaya ya Magharii “A”.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (wa pili kushoto) alipokuwa akizungumza na Wajenzi wa Kampuni ya Ujenzi wa Tangi la Maji Safi na Salama “Mehga Ingeneering &Instruction  LTD “ambayo imeahidi kumalizika kwa ujenzi huo ifikapo Mwezi januari Mwakani,wakati wa ziara ya kutemelea na kuangalia miradi mbali mbali ya maendeleo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi alipokuwa akimsikiliza Bibi Raifa Kibwana Mkaazi wa Dole, Wilaya ya Magharibi A akizungumzia changamoto zinazowakabili katika Shehia yao wakati wa ziara ya   kutembelea na kuangalia miradi mbali mbali ya maendeleo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi alipokuwa akizungumza na Wananchi wa Mwera wakati alipozindua ujenzi wa Barabara za Vijijini kwa kiwango cha lami,alianzia barabara ya  Mwera -Kibondemzungu  wakati wa ziara ya   kutemelea na kuangalia miradi mbali mbali ya maendeleo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto )alipokuwa akisisitiza jambo wakati alipoisimamisha kazi Kampuni ya Assosiated Investiment& Services  LTD ya Dar Es Salaam chini ya usimamizi wa Nd,Theodony Andrew  Zani  kutokana na utendaji wao wakazi wa kusuasua katika Shehia ya Monduli   akiwa katika  ziara ya   kutembelea na kuangalia miradi mbali mbali ya maendeleo kwa Wilaya ya Magharibi “A”Mkoa wa Mjini Magharibi.[Picha na Ikulu] 16/07/2022.
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad