HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 2, 2022

MTAMBO WENYE THAMANI YA BILIONI 1.5 WAZIMDULIWA HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA

 

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, akikata utepe kuzindua mwongozo wa utoaji dawa wa Hospitali ya Benjamin Mkapa katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Dkt Deo Mtasiwa na Dkt Alphonce Chandika, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akizindua  jengo la mitambo ya oksijeni Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini DodomaNa Janeth Raphael.

WAZIRI wa Afya Ummy mwalimu ametoa Rai Kwa hospitali ya Benjamin mkapa na hospitali zote nchini kutunza raslimali zinazowekekezwa kwenye hospitali zote hapa nchini.

Akizindua Mtambo wa uzalishaji Hewa Tiba ya Oksijeni wenye Thamani ya shilling billion 1.5  leo jijini Didoma waziri Ummy amesema kukamilika kwa usimikaji wa mitambo hiyo hatua inayofuata ni kuisimamia uendeshaji na utunzaji wa Rasilimali hizo.

"Tutapita kukagua kama hilo limetekelezwa na pale itakapotokea tatizo na ikabainika kuwa ni uzembe au hujuma za makusudi za baadhi ya Watumishi wenzetu hatua za kinidhamu zitachukuliwa" Amesema Mh ummy mwali waziri wa Afya.

Aidha,waziri ummy amesema serikali imesitisha Matumizi ya Fomu za Bima ya Afya (Form 2C) ambazo zilikuwa zinaruhusu watu kukosa dawa hospitali  na kwenda kwenye vituo vya nje kununua dawa.

"Niwaombe wagonjwa hasa wale wanachama wa mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) Na watoa huduma kwenye hospital zetu za Rufaa za mikoa kushirikiana na wizara katika zoezi la kusitisha matumizi ya Form 2C kuanzia leo julai mosi tumesitisha Rasmi  Matumizi ya Fomu za Bima ya Afya ambazo zilikuwa zinaruhusu watu wanapokosa dawa kwenye vituo vya Afya kwenda kununua kwenye vituo vingine nje" Amesema waziri wa Afya Ummy Mwalimu.

Kwa upande wake Dkt Alphonce Chandika, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospital ya Benjamini Mkapa amesema Mtambo uliozinduliwa umegharimu kiasi cha shilling Billion 1.5 ambapo Mtambo huo unauwezo wa kuzalisha Mitungi 400 kwa siku.

"Tangu Tulipoanza uzalishaji wa Majaribio Tarehe 8 january 2022 hadi sasa Mtambo huu umezalisha Mitungi 8,373 yenye Thamani ya shillingi 418,650,000 kutokana na bei Tuliyokuwa Tukinunulia kwenye soko" Amesema Dkt Alphonce chandika.

Dkt chandika amesema uwepo wa Mtambo huo umeweza kuokoa pesa za serikali jumla ya shillingi 396,895,709 ambapo mitungi hiyo ingenunuliwa kutoka kwenye viwanda Binafsi kwani gharama za uzalishaji zilizotumika katika kipindi hiki ni 21,754,291.

Dkt Deodatus Mtasiwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya hospital ya Benjamini Mkapa ameiahidi serikali kuwa wataitunza Mitambo hiyo pamoja na kuitumia kwenye malengo yaliyokusudiwa ili kutoa huduma Bora kwa Wananchi.
Wakwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Tiba toka Wizara ya Afya, Dkt. Omary Ubuguyu, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dkt Deo Mtasiwa, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, Mkurugenzi  Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dkt Alphonce Chandika, Mkuu wa Kliniki ya Kinywa na Meno wa BMH, Dkt Alex Kimambo, wakiwa kwenye Mtambo wa Hewa Tiba ya Oxygen wa BMH
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt Alphonce Chandika akizungumza katika uzinduzi huo.
WAZIRI Ummy Mwalimu akizungumza katika uzinduzi huo
Mtambo wa uzalishaji hewa uliozinduliwa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma wenye Thamani ya shilingi bilioni 1.5

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt Alphonce Chandika akimuonyesha waziri wa Afya Ummy Mwalimu Sehemu ya mtambo huo uliozinduliwa.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, akionyesha Kitabu cha Mwongozo wa kutoa Dawa cha Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) alichokizundua leo, wanaoangalia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya BMH, Dkt Deo Mtasiwa, kulia na Mkurugenzi wa Tiba toka Wizara ya Afya, Dkt Omary Ubuguyu (Kushoto)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad