HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, July 24, 2022

MAKAMU WA RAIS UZINDUZI WA MRADI WA MAJI SIBWESA

 

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amezindua mradi wa maji wa Sibwesa uliopo Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi, mradi uliogharimu shilingi milioni 173.2 ukiwanufaisha wananchi zaidi ya elfu saba wa Kijiji cha Sibwesa.

Mradi huo ni kati ya miradi ya maji iliotekelezwa kwa kutumia fedha za ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya Uviko19.

Akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Tanganyika mara baada ya kuzindua mradi huo, Makamu wa Rais amesema serikali itaendelea kutekeleza miradi muhimu ya huduma za kijamii kama vile maji, elimu na afya ili kuwasaidia wananchi kufikia maendeleo ya haraka.

Mradi huo umewezesha kupatikana kwa maji safi na salama katika taasisi zote zilizopo eneo la sibwesa pamoja na kuwasaidia wananchi kuondokana na maradhi yatokanayo na maji yasio safi yalikuwa yakipatikana hapo awali.

Akiwa katika Kijiji cha Sibwesa Makamu wa Rais ameagiza kupelekwa kwa mtaalamu wa kilimo katika Kijiji hicho ili kuweza kuwasaidia wananchi kufanya kilimo cha kisasa na kuongeza uwingi wa upatikanaji wa mazao.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maji mheshimiwa Maryprisca Mahundi amesema sera ya wizara ya maji ni kuhakikisha huduma ya maji inafikishwa katika taasisi zote za kiserikali na zisizo za kiserikali. Amesema pamoja na uwepo wa mradi huo serikali inatarajia kutekeleza mradi wa shilingi bilioni 1.8 ili kusaidia wilaya hiyo katika vijiji vine vya vya Nkungwi, Kasekese, kaseganyama na Sibwese.

Mwakilishi wa wananchi ambaye ni mbunge wa Mpanda vijijini Selemani Kakoso ameipongeza serikali kwa kutekeleza mradi huo ambao umepelekea mabadiliko makubwa katika Kijiji hapo na kuwawezesha wanafunzi kutumia kikamilifu mud awa masomo tofauti na awali walipokuwa wakitafuta huduma ya maji muda mwingi. Ameiomba serikali kuisaidia wilaya ya Tanganyika na mkoa wa Katavi kwa ujumla kuondokana na changamoto ya maji kwa kutumia ziwa Tanganyika ambalo ni chanzo cha uhakika cha maji.

Katika hatua nyingine Makamu wa Rais akiwa ziarani katika Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi amewasalimia wananchi wa Kijiji cha kayenze na kuiagiza wizara ya maji kuhakikisha mradi wa maji katika Kijiji hicho unakamilika ifikapo mwezi desemba mwaka huu kutokana na serikali kumlipa fedha mkandarasi anaetekeleza mradi lakini bado mradi ukiendelea kusuasua.

Akiwa katika Kijiji cha Centre Maria, Makamu wa Rais ameigiza wizara ya Nishati kuhakikisha inatatua changamoto ya kukatika kwa umeme katika eneo hilo na Katavi kwa ujumla ikiwemo kupeleka Jenereta itakayoongeza upatikanaji wa umeme katika mkoa huo. Makamu wa Rais amewahimiza wananchi wa eneo hilo kuzingatia suala la lishe licha ya kwamba wanaongoza katika uzalishaji wa mazao ya chakula nchini.

Aidha amewaagiza kulinda na kuhifadhi mazingira ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi yanayosababisha madhara mbalimbali kama vile ukame na joto kupita kiasi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad