HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 29, 2022

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS AFANYA MAZUNGUMZO NA KIKOSI KAZI CHA KUKUSANYA MAONI KUHUSU MAGEUZI YA SEKTA YA ELIMU

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amekishauri Kikosi Kazi kinachokusanya maoni ya wadau kuhusu Mageuzi ya Sekta ya Elimu nchini kufikiria kwa mapana zaidi na kuelekeza mtazamo wa mwelekeo wa dunia unazingatia sana suala la ubunifu na uvumbuzi wa teknolojia katika maendeleo ya elimu.

Mhe. Othman ameyasema hayo ofisini kwake Migombani mjini Zabzibar alipokutana na kikosi Kizi kinachokusanya maoni ya wadau kuhusu mageuzi ya sekta ya Elimu Zanzibar kinachoongwa na Makamu Mkuu Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Profesa Ahmada Rai.

Amefahamisha kwamba kutokana na mwelekeo wa dunia ulivyo ni muhimu kufahamu mahali na uwezo wanchi kitaaluma sambamba na kujua matarajio ya unapohitaji kufikia katika mageuzi hayo ili kuweza kufanya uwekezaji wa maeneo muhimu yote yanayohitajika katika sekta hiyo.

Amefafanua kwamba hatua ya kufikiri mageuzi hayo kwa mapana ni pamoja na kuwa na muono wa kufahamu kwamba elimu itakayofundishwa katika ngazi mbali mbali nchini inauwezo wa kuzalisha wataalamu wa fani tofauti watakaofanyakazi kwa ujunzi na marifa makubwa na kuweza kushindanishwa na wataalam wanaotoka sehemu yoyote ile dunaini.

Ametolea mfano wa mwalimu atakayezalishwa kwenye Vyuo vya Zanzibar kufikiria mageuzi ya kumuandaa ambaye ataweza kufundisha na kukubalika kiuwezo katika nchi yoyote ndani ya Afrika ama kwengineko duniani.

Aidha amesema kwamba kunahaja pia ya kuziangatia kwa makini suala la matakwa ya kitaaluma kwa waajiri wa sekta mbali mbali za maendeleo wakiwemo sekta binafsi kwa kuwa wao ndio watumiaji wakubwa wa wataalamu wanaozalishwa ndani na nje ya nchi.

Amefahamisha kwamba mweleleko wa megeuzi unaohiotajika pia ni kuwajenga walimu kiuwezo , heshima na maslahi yao ya aina mbali mbali kwa kuwa bila kuwajenga vyema walimu taifa haliwezi kusonga mbele.

Aidha amewataka pia kuutumia uzoefu uliotumika katika sekta nyengine nchini ili usaidie kutoa mweleko juu ya mabadiliko muhimu yanayohitajika ambayo yatachangia kuleta mageuzi stahiki katika sekta ya elumu hapa Zanzibar kama matarajio ya serikali yalivyo sasa.

Pia mhe. Othman ameshauri kuangaliwa suala la wajibu na jukumu makhusi kwa mzazi katika kuchangia maendeleo ya elimu kwa mtoto ili shughuli ya upatikanaji wa elimu kwa mtoto iwejumishi.

Kwa upande mwengine ameshauri pia kuangalia mchango wa sekta binafasi katika elimu ikiwa ni pamoja na kuwepo motisha kwa wamiliki wa skuli binafsi kwa kuwa ni wadau na washirika muhimu katika kuchangia maendeleo ya elimu nchini sambamba na kuipunguzia mzigfo serikali.

Naye Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Ali Abdulgulam Hussein, amesema kwamba Kikosi hicho chenye wataalamu mahiri kimeaminiwa na Serikali na kimepewa jukumu kubwa la kupendekeza hatua mbali mbali za mageuzi yanayohitajika katika sekta ya elimu nchini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kikosi Kazi hicho Profesa Ahamada Rai, amesema kwamba tayari kikosi kimeanza kukutana na wadau mbali mbali katika kuendeleza kazi ya kukusanya maoni ya kupendekeza mageuzi makubwa yanayohitajika katika sekta ya elimu Zanzibar.

Amesema kwamba azma ya serikali ya kutaka kuleta mageuzi kwenye sekta ya elimu Zanzibar ni kutokana na changamoto kadhaa zilizopo ndani ya mfumo wa elimu Zanzibar na kwamba tayari wamejifunza kuufahamu mfumo wa uliopo sasa kupitia vikao na wadau mbali m tena kwa wadau kabla ya kuwasilishwa serikalini.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman , akizungumza na Kikosi Kazi cha kukusanya maoni kuhusu mageuzi katika sekta ya elimu Zanzibar. Mazungumzo hayo yalifanyika ofisini kwa kwa makamu Migombani mjini Zanzibar wakati kamati hiyo ilipofika kupata maoni yake tarehe 28.07.2022. Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kitengo cha habari.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman , akizungumza na Kikosi Kazi cha kukusanya maoni kuhusu mageuzi katika sekta ya elimu Zanzibar. Mazungumzo hayo yalifanyika ofisini kwa kwa makamu Migombani mjini Zanzibar wakati kamati hiyo ilipofika kupata maoni yake tarehe 28.07.2022. Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kitengo cha habari.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman , akizungumza na Kikosi Kazi cha kukusanya maoni kuhusu mageuzi katika sekta ya elimu Zanzibar. Mazungumzo hayo yalifanyika ofisini kwa kwa makamu Migombani mjini Zanzibar wakati kamati hiyo ilipofika kupata maoni yake tarehe 28.07.2022. Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kitengo cha habari.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman , akianganba na Mwenyekiti wa Kikosi Kazi cha kukusanya maoni kuhusu mageuzi katika sekta ya elimu Zanzibar Profesa Ahmada Rai nje ya Ofisi ya Makamu baada ya kumaliza mzungumzo yalifanyika ofisini kwa kwa makamu Migombani mjini Zanzibar wakati kamati hiyo ilipofika kupata maoni yake tarehe 28.07.2022. Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kitengo cha habari.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman , akianganba na Mjuumbe Kamati ya Kikosi Kazi cha kukusanya maoni kuhusu mageuzi katika sekta ya elimu Zanzibar Dk. Said Gharib Bilali nje ya Ofisi ya Makamu baada ya kumaliza mzungumzo yalifanyika ofisini kwa kwa makamu Migombani mjini Zanzibar wakati kamati hiyo ilipofika kupata maoni yake tarehe 28.07.2022. Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kitengo cha habari

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad