KONGAMANO LA SHINA INC KUFANYIKA DODOMA MWAKA 2023 - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 6, 2022

KONGAMANO LA SHINA INC KUFANYIKA DODOMA MWAKA 2023

 

Kongamano la Vijana linaloandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la SHINA INC linatarajiwa kufanyika Dodoma mwaka 2023 hii ni kuendeleza kutoa elimu ya utambuzi kwa vijana mbalimbali hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Rais wa Shirika la SHINA INC, Jesca Mushala wakati akifunga Kongamano la Vijana lililofanyika Makunduchi, Zanzibar kuanzia tarehe 24 hadi 27 Juni mwaka 2022.

Amesema kuwa Kongamno lijalo litafanyika Dodoma kwasababu kuu tatu , kwanza ni makao makuu ya Nchi, Pili kuna viongozi wengi wa Serikali Dodoma, tatu kuna vyuo vingi Dodoma, nne wengi wa Wanakongamano hawajawahi kufika Dodoma , tano tutaweza kuwa na uhuru wa kukutana na wabunge mbalimbali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuweza kutoa mawazo mbalimbali watakayoyawasilisha Bungeni.

“Kama tutakwenda Dodoma Sheria zitakuwa kali zaidi kuliko Makunduchi hii yote ni kwasababu tumejifunza kitu kwenye Kongamano hili.” Alisema Mushala

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad