KONGAMANO LA SENSA LAFANYIKA ZANZIBAR - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, July 31, 2022

KONGAMANO LA SENSA LAFANYIKA ZANZIBARRahma Khamis –Maelezo Zanzibar

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Ikulu Mhe, Jamal Kassim Ali amesema muelekeo wa Taifa ni kufanya Sensa ya watu na makazi ifikapo Agost 23 mwaka huu ili Serikali zote mbili kuweza kuwasaidia wananchi wake baada ya kupata takwimu sahihi nchini.

Akizungumza kwa niaba yake mara baada ya kufungua kongamano la Sensa na Uchumi liliowashirikisha vijana katika Ukumbi wa Shekh Idriss Abdulwakil, Mkurugenzi Utumishi na Uendeshaji Afisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Suleiman Moh’d Rashid amesema kuwa ni utaratibu uliopangwa na Serikali kujua idadi ya watu na makaazi kila baada ya kipindi ili kuweza kupanga mipango madhubuti ya kuwahudumia wananchi wake.

Amesema miongoni mwa umuhimu wa kufanya Sensa ya watu na makazi ni pamoja nakuiwezesha Serikali kusambaza huduma muhimu za jamii ikiwemo maji na Afya ambazo ni lazima wananchi kuzipata .

Aidha,amewaomba wananchi kuwa tayari kuhesabiwa kwani upatikanaji wa twakim za uhakika kutasaidia kueneza huduma hizo katika maeneo husika .

Alifafanua kuwa suala la Sensa ya watu na makazi halihusiani na chama, dini rangi wala kabila bali ni la kitaifa hivyo ni haki ya kila mtu kushiriki zoezi la kuhesabiwa na kuwaasa wananchi kuachana na dhana potofu juu ya kushiriki zoezi hilo.

Nae Mwenyekiti wa Taasisi inayoshughulikia maendeleo ya uchumi kwa vijana (MAYODA ECONOMIC DEVELOPMENT GROOP) Agustino Osca Matefu amesema kuwa lengo la kuanzisha taasisi hiyo ni kuwawezesha vijana kwa kuwajengea uwezo na kuwapatia mitaji ili kuwainua kiuchumi.

Amesema kuwa wameamua kufanya kongamano la Sensa na Uchumi kwa lengo kuwahamasisha na kuwachochea vijana kushiriki katika zoezi la Sensa ya watu na makazi na kukubali kuhesabiwa ili kuuunga mkono juhudi za Serikali zote mbili.

Aidha Mwenyekiti huyo ameomba kupatiwa eneo la kujenga Ofisi Zanzibar ili vijana waweze kufanya kazi na kufikia malengo kupitia fursa mbalimbali zinazopatikana katika taasisi hiyo.

Nao washiriki katika kongamano hilo walishukuru taasisi hiyo kwa kupatiwa elimu hiyo na kuahidi kuwa wataifanyia kazi kwa kuwahamasisha wananchi mbalimbali kushiriki katika zoezi la kuhesabiwa .

Kongamano hilo ni la siku moja lilioandaliwa na (MAYODA ECONOMIC DEVELOPMENT GROOP) ambapo mada mbalimbali zilijadiliwa ikiwemo Sensa, Makazi na Ajira. 

Mkurugenzi Utumishi na uendeshaji Afisi ya Rais Fedha na mipango Zanzibar Sleiman Mohammed Rashid  akipokea tunzo  maalum ya utendaji kazi bora ya  Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Husein Ali Mwinyi kutoka Kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya MAYODA Economic Development Group wakati wa kongamano la  Sensa na Uchumi lilowashirikisha Vijana huko Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdul-wakil Kikwajuni Mjini Zanzibar.PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad