BENKI YA DCB YACHANGAMKIA FURSA ZA UWEKEZAJI KATIKA UCHUMI WA BULUU VISIWANI ZANZIBAR - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 11, 2022

BENKI YA DCB YACHANGAMKIA FURSA ZA UWEKEZAJI KATIKA UCHUMI WA BULUU VISIWANI ZANZIBAR

 

 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Dk. Saada Mkuya (katikati), akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Godfrey Ndalahwa (kushoto), na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Bi. Rahma Ngassa katika mkutano aliouandaa akiwashirikisha wakuu wa taasisi mbalimbali za fedha za bara na visiwani kujadili fursa mbalimbali za kifedha zipatikanazo katika kampeni ya uchumi wa buluu iliyoasisiwa na Rais wa nane wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi. Hafla hiyo ilifanyika visiwani humo jana. Uchumi wa Buluu ni dhana inayohusisha uchumi unaojijenga katika Utalii, Uvuvi, Mafuta, gesi na viwanda vinavyotumia malighafi za bahari.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Godfrey Ndalahwa akizungumza huku wajumbe wengine wakimsikiliza katika mkutano uliandaliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Dk. Saada Mkuya (hayupo pichani), ukiwashirikisha wakuu wa taasisi mbalimbali za fedha za bara na visiwani kujadili fursa mbalimbali za kifedha zipatikanazo katika kampeni ya uchumi wa buluu iliyoasisiwa na Rais wa nane wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi inayoendelea visiwani humo. Hafla hiyo ilifanyika mjini Zanzibar jana. Uchumi wa Buluu ni dhana inayohusisha uchumi unaojijenga katika Utalii, Uvuvi, Mafuta, gesi na viwanda vinavyotumia malighafi za bahari.

 Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya DCB, Rahma Ngassa akishiriki pamoja na washiriki wengine mkutano uliandaliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Dk. Saada Mkuya (hayupo pichani), ukiwashirikisha wakuu na wawakilishi wa taasisi mbalimbali za fedha za bara na visiwani kujadili fursa mbalimbali za kifedha zipatikanazo katika kampeni ya uchumi wa buluu iliyoasisiwa na Rais wa nane wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi inayoendelea visiwani humo. Hafla hiyo ilifanyika mjini Zanzibar jana. Uchumi wa Buluu ni dhana inayohusisha uchumi unaojijenga katika Utalii, Uvuvi, Mafuta, gesi na viwanda vinavyotumia malighafi za bahari.Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Godfrey Ndalahwa (katikati, akipozi katika picha pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Dk. Saada Mkuya (wa tatu kushoto) pamoja na wakuu na wawakilishi wa taasisi mbalimbali za fedha kutoka bara na visiwani mara baada ya mkutano ulioandaliwa na mheshimiwa waziri kujadili fursa mbalimbali za kifedha zipatikanazo katika kampeni ya uchumi wa buluu iliyoasisiwa na Rais wa nane wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi inayoendelea visiwani humo. Hafla hiyo ilifanyika mjini Zanzibar jana. Uchumi wa Buluu ni dhana inayohusisha uchumi unaojijenga katika Utalii, Uvuvi, Mafuta, gesi na viwanda vinavyotumia malighafi za bahari.
No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad