HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 29, 2022

WHO na Manyara kutembea nyumba kwa nyumba kutoa chanjo ya UVIKO 19

 


Na John Walter-Manyara
Mkoa wa Manyara kwa kushirikiana na Shirika la Afya Ulimwenguni, WHO, kwa pamoja na wadau mbalimbali wameanza kampeni maalum ya kuwachanja wananchi wa mkoa huo dhidi ya COVID-19 kwa kutembea nyumba kwa nyumba ili kuwafikia watu wa jamii zote na walio katika mazingira magumu.

Katika zoezi la kuchanja wananchi dhidi ya ugonjwa huo ambao umepoteza maisha ya wengi na kuwaacha wengi wakiwa yatima na wajane, mkoa wa Manyara unatajwa kushika nafasi ya mwisho kitaifa kuchanja raia wake.
Katibu tawala mkoa wa Manyara Karolina Mthapula amesema wamejipanga kuhakikisha wanafikia lengo.
Hadi sasa mkoa wa Manyara umetoa chanjo kwa watu takribani laki tatu, idadi ambayo ni sawa na asilimia 3.7 tu ya lengo.

Akizungumza mjini Babati wakati wa kikao kazi cha tathmini ya utoaji chanjo ya UVIKO -19, Meneja wa mpango wa chanjo wa Taifa kutoka wizara ya Afya Dkt. Florian Tinuga amesema hadi sasa mkoa wa Ruvuma ndio unaoongoza kitaifa kwa kufikia asilimia 40 ya uchanjaji.

Ikumbukwe kuwa Lengo la kitaifa ni kufikia asilimia 70 ya kutoa chanjo dhidi ya UVIKO -19 ifikapo mwezi Desemba mwaka huu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi kutoka shirika lisilo la kiserikali la JHPIEGO, Maryrose Giattas amesema shirika lake litatoa zaidi ya shilingi bilioni moja kuunga mkono kampeni ya chanjo dhidi ya UVIKO-19 mkoani Manyara.

Naye mkuu wa mkoa wa Manyara, Makongoro Nyerere amewataka watendaji mkoani humo kuhamasisha wananchi ili wajitokeza na kupata chanjo dhidi ya UVIKO -19.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad