HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 1, 2022

Wezi wavamia na kuiba Mil 2 kwenye nyumba ya watawa wa kike (MASISTER)

 


Na Amiri Kilagalila,Njombe
TUKIO hili limetokea eneo la Emiliwa halmashauri ya mji wa Njombe kituo cha masister wa kanisa la Roman Katoliki katika jengo ambalo watawa wa kike wanalitumia kwa ajili ya wakala wa fedha.

Amebainisha hayo kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa wakati akifafanua namna wizi huo ulivyotokea juzi Mei 30 majira ya saa 12 jioni.

“Vijana wanne walifika eneo la masister na mmojawao akawa anaongea nao kama vile anahitaji huduma akataja kiwango kikubwa na wale wakawa wanahesabu kama kipo ndipo akawaita wenzake wakaja na silaha aina ya bunduki wakachukua hela kiasi cha milioni mbili na kuanza kukimbia”alisema Kamanda Issa

Aidha amesema jeshi la polisi limefanikiwa kuwakamata vijana wawili kati yao walioshindwa mara baada ya kuanguka katika piki piki na kuanza kushambuliwa na wananchi.

“Wakati wanakimbia kuna sehemu kumewekwa magogo walianguka,cha ajabu mmoja alibeba pikipiki na kuanza kukimbia nayo wakati hawa wengine wakabakia ndipo waliposhambuliwa na wananchi”alisema Kamanda

Kamanda Issa amesema jeshi hilo linaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini walipo vijana wengine huku akiwashukuru na kuwapongeza wananchi kwa kuhakikisha uhalifu unadhibitiwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad