VIONGOZI WA MUSODCC WAAPISHWA, WAASWA KUSHIRIKIANA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 1, 2022

VIONGOZI WA MUSODCC WAAPISHWA, WAASWA KUSHIRIKIANA

Rais wa Serikali ya Wanafunzi (MUSODCC),Ombeni Kisuka akiapishwa na Mwanasheria kutoka Chuo Kikuu Mzumbe ndaki ya Dar es Salaam, Nora Msuya leo Juni Mosi, 2022.

Baadhi ya Viongozi mbalimbali wa Serikali ya wanafunzi ndaki ya Dar es Salaam wakiapishwa na Mwanasheria wa Chuo Kikuu Mzumbe ndaki ya Dar es Salaam, Nora Msuya mara baada ya kushinda uchaguzi wa 2021/2022.
Rais wa Serikali ya Wanafunzi (MUSODCC)aliyemaliza Muda wake, John Baraka akizungumza mara baada ya viongozi wapya wa serikali ya wanafunzi kuapishwa leo Juni Mosi, 2022 katika Ndaki ya Dar es Salaam.

Mshauri wa Wanafunzi Zitta Mnyanyi akizungumza wakati wa kuwaapisha viongozi wa serikali ya wanafunzi wa Ndaki ya Dar es Salaam leo Juni Mosi, 2022 jijini Dar es Salaam.
Rais wa Serikali ya Wanafunzi aliyemaliza Muda wake(MUSODCC), John Baraka akizungumza mara baada ya viongozi wapya wa serikali ya wanafunzi kuapishwa leo Juni Mosi, 2022 katika Ndaki ya Dar es Salaam.
Rais wa Serikali ya Wanafunzi aliyemaliza Muda wake (MUSODCC), John Baraka akimkabidhi lisala Kaimu Mkuu wa Ndaki ya Dar es Salaam Dkt. Coretha Komba kabla ya kuwaapisha viongozi wapya wa serikali ya wanafunzi leo Juni Mosi, 2022 katika Ndaki ya Dar es Salaam.
Rais wa Serikali ya Wanafunzi aliyemaliza Muda wake(MUSODCC), John Baraka akimkabidhi Rais wa Serikali ya Wanafunzi (MUSODCC),baadhi ya nyaraka ambazo zitawaongoza katika kuongoza serikali hiyo ya wanafunzi jijini Dar es Salaam leo Juni Mosi, 2022.

Kaimu Mkuu wa Ndaki ya Dar es Salaam Dkt. Coretha Komba akizungumza na uongozi mpya wa serikali ya wanafunzi wa Ndaki ya Dar es Salaam (MUSODCC) leo Juni Mosi, 2022 jijini Dar es Salaam.
Rais wa Serikali ya Wanafunzi (MUSODCC),Ombeni Kisuka akisaini moja ya nyara mara baada ya kuapishwa kwa nafasi hiyo kwaajili ya kuongoza mwaka wa masomo wa 2022/2023.
Mwanasheria wa Chuo Kikuu Mzumbe ndaki ya Dar es Salaam, Nora Msuya akizungumza mara baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali wa serikali ya wanafunzo wa Ndaki ya Dar es Salaam (MUSODCC) leo Juni Mosi, 2022.
Baadhi ya viongozi wa MUSODCC wakiwa katika uapisho wa viongozi wapya wa serikali hiyo.


Picha za pamoja.

CHUO Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam kimewaapisha Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi (MUSO DCC) ambao wameshinda katika uchaguzi wa Viongozi mara baada ya Uongozi Uliopita Kumaliza Muda wake.

Uchaguzi huo katika ndaki ya Dar es Salaam, ulifanyika Mei, 26,2022 katika Kituo Cha Tegeta na Upanga.

Viongozi hao wapya wataongoza kwa Mwaka Mmoja wa 2022/2023 ambapo watamaliza muda wao.

Walioapishwa leo ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi (MUSO DCC), Ombeni Kisuka aliyeshinda kwa kura 135 baada ya kuwashinda Carren Njogoro na Abdallah Omar.

Na katika nafasi ya Makamu wa Rais, Zauda Halisi ameshika nafasi hiyo baada ya Mgombea wa Urais Kisuka kuibuka Mshindi.

Katika nafasi ya Mwakilishi wa Seneti, Zephani Malembele ameapishwa mara baada ya kushinda nafasi hiyo kwa kura 265.

Kaimu Mkuu wa Ndaki ya Dar es Salaam Dkt. Coretha Komba akizungumza mara baada ya kuapishwa amewaasa kuongoza huku wakijua kuwa wao ni Wanachuo.

Amesema kuw akiongozi mzuri ni yule ambaye anafaulu mitihani Vizuri bila kuwa na kipolo katika mitihani pia amewaasa kushirikiana na Viongozi wengine wa Mzumbe ili kuleta maendeleo yenye tija kwa jamii nzima wa Wanamzumbe.

Kwa Upande wa Mwanasheria kutoka Chuo Kikuu Mzumbe ndaki ya Dar es Salaam, Nora Msuya amesema kuwa huo ndio mwanzo wa kuwa viongozi wazuri au wabaya hivyo wanatakiwa kufata misingi ya uongozi.

Amesema kuwa pia hata waliyoifikia ni hatu nzuri wajitahidi huko baadae waje kugombea nafasi za uongozi wa siasa serikalini.

Kwa Upande wa Rais wa Serikali ya Wanafunzi (MUSODCC), Ombeni Kisuka amesema uongozi wake utakuwa wa kushirikisha kati ya wanafunzi, Viongozi wa chuo na Viongozi wa MUSO.

Kwa Upande wa Rais Mstaafu wa Serikali ya wanafunzi, John Baraka amewatakia uongozi mwema katika kuongoza Wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam.

Aidha amewaasa viongozi wapya Kutoa taarifa kwa wanachuo wengine pale zinapotokea ili kila mwanafunzi awe na taarifa kwa kile kinachoendelea.

Akiwapongeza Viongozi wa MUSO DCC, mshauri wa Wanafunzi Zitta Mnyanyi amewapa hongera kwa nafasi waliyoipata pia amewashauri wakaongoze kwa weredi wanafunzi wenzaao bila kuwa na ubaguzi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad