HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, June 20, 2022

Ukoo wa Mallya washtukia Ujambazi, mauaji, ubakaji, wakaa na Vijana wao kuwaponya

JAMII imetakiwa kuwaongoza na kuwaelekeza vijana tulikotoka na tunapoelekea ili kujenga Taifa imara lenye umoja, mshikamano, chapakazi na lenye maadili mema.

Hayo yameelezwa leo na Mwenyekiti wa ukoo wa Mallya Meja Thomas Mallya wakati wa sherehe ya Kishari ya Ukoo huo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Meja Mallya amesema, ili kuponya jamii ya sasa hasa viijana kuna haja ya kuwa na vikundi hivyo vya aina hiyo ili kuwaweka vijana pamoja na kuwapa maarifa ya namna ya kujikwamua kiuchumi na kuhimiza maadili kwa ujumla.

‘’Lazima kuwaeleza vijana wetu ni wapi tumetoka na tulipo ili kujenga jamii yenye maadili…kwa sasa vijana wadogo wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kucomment vitu bila kujua chimbuko lake, sisi wazee wa ukoo wa Mallya tukaona ni vyema kuwa na umoja huu katika kushirikiana na kuwasaidia vijana kwa kuwajenga ili kuwa na kizazi bora kwa sasa na baadaye.’’ Amesema.

Kuhusana na matukio ya mauaji yanayotokea katika maeneo mbalimbali nchini Meja Mallya amesema, jamii ikiacha vijana wafundwe na ulimwengu wimbi la ubakaji na ujambazi litakuwa kubwa hivyo vikundi kama hivyo vilenge kuwaelekeza kama ilivyokuwa vikundi vya machifu vilivyoanzishwa ili kulinda familia, wajukuu, koo na vizazi.

Aidha amewaomba viongozi wa dini kushirikiana na Serikali katika kulinda tunu ya amani kwa kuhubiri amani katika jamii hasa katika kipindi hiki ambacho upendo umelega hali inayopelekea ndugu kwa ndugu kuuwana kutokana na kukosa hofu ya Mungu na maadili.

Awali Katibu Mwenezi wa kikundi cha kijamii cha ukoo wa Mallya Anthony Mallya ameeleza kuwa, vijana hueleza matatizo yao kwa watu wa karibu na waliowazoea na kuwaeleza changamoto zinazowakabili.

‘’Vikundi vya namna hii vina umuhimu sana katika kushirikiana katika shida na kuongoza vijana katika maadili mema ni vyema matabaka na koo kuwa na vikundi vya namna hii ili kutokomeza matukio ya uhalifu na hata vijana wataogopa kushiriki vitendo vya namna hiyo kwa kuwa wazazi, ndugu na wanajamii wapo katika vikundi hivyo ambavyo vinasimamia maadili na kuwaweka pamoja…..Malezi huanzia nyumbani hatupaswi kuilamu Serikali tuhakikishe tunashirikiana katika kujenga vijana weledi, wachapakazi na wenye maadili’’ Amesema.

Awali akitoa taarifa ya umoja huo Katibu wa Kishari hicho Evarist Theodori amesema kuwa umoja huo umekuwa ukienzi yaliyokuwa yakifanywa na babu zao kwa kukutana pamoja, kushirikiana katika shida na raha pamoja kushirikishana shughuli za kiuchumi ikiwemo kilimo ambapo hadi sasa kila familia ya Mallya Kibosho Magharibi, Moshi vijijini imefikiwa na huduma ya maji safi na salama.

Amesema, ni muhimu kwa vijana kuwa na vikundi vitakavyowasaidia kijamii na kiuchumi pamoja na kuwa na sehemu ya kutatua changamoto zao kwa kuomba ushauri kwa wazee wa Kishari na kuwaomba akina Mama kuendelea kuwaongoza vyema katika maadili na nidhamu.

Sikiliza Maoni ya Wazee wa Ukoo wa Mallya 


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad