HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, June 11, 2022

TUBOFESHE VYUO VYETU VYA KATI ILI VIJANA WATAKAOSHINDWA KUENDELEA NA MASOMO YA SEKONDARI WAKASOME HUKO.

 

Waziri Dkt Jafo Wakati akuhutibia KATIKA uzinduzi wa MAONYESHO ya elimu ya sayansi na MAFUNZO ya ufundi stadi ( TVET).

Waziri wa nchi Ofisi yae Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt.Seleman Jafo (Wa kwanza kulia) sambamba na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda (wa pili kulia) wakiwa wametembelea moja ya mabanda yaliyopo katika maonesho hayo.
Waziri Dkt.Seleman Jafo (katikati) sambamba na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda (kushoto)  wakiwa wametembelea moja ya mabanda yaliyopo katika maonesho hayo.
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Selemani Jafo amemuakilisha Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango kuwa mgeni rasmi katika maonesho hayo yanafanyika jijini Dodoma katika uwanja wa Jamhuri Kushoto ni Waziri wa elimu sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka.

Na Janeth Raphael
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Mazingira na Muungano Dkt Seleman Jafo amewataka vijana wanaomaliza elimuya kidato cha nne na kushindwa kuendelea na kidato cha tano kujiunga na vyuo vya kati na ufundi.

Waziri Dkt Jafo aliyasema hayo jijini Dodoma wakati akifungua maonesho ya Elimu ya Sayansi na mafunzo ya ufundi stadi (TVET).

Dkt Jafo amesema takwimu za mwaka jana zinaeleza kuwa wanafunzi 173000 walimaliza kidato cha nne kati yao wanafunzi 90,000 waliendelea na masomo ya kidato cha tano na sita.

“Leo hii kuna vijana wengi wanamaliza kidato cha nne lakini sio wengi wanaoendelea na kidato cha tano na sita vlazima tuboreshe vyuo vyetu vya kati ili vijana ambao watashindwa kuendelea na masomo waende katika vyuo vya kati na ufundi,”alisema

Dkt Jafo amesema serikali ya awamu ya sita imewekeza katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo itatanua wigo wa kuajiri vijana wenye umahili katika ufundi.

Alisema Tanzania inafanya uwekezaji mkubwa katika ujenzi wa bwawa la kufua umeme la mwalimu nyerere ambalo ujenzi wake unaendelea na utahitaji vijana ambao wana ujuzi wa kutosha.

“Maeneo ambayo Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uwekezaji mkubwa yanahitaji vijana ambao wamepata elimu ya ujuzi na sasa imeanza mchakato wa kufufua shirika la ndege ambapo hadi sasa kuna ndege 11 na itanunua nyingine hivyo wataitajika vijana wenye ujuzi wa katika uendeshaji na ukarabati wa vifaa hivyo,”alieleza.

Kwa upande wake Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda amesema kuwa serikali ili kuendelea kukuza bunifu za wanafunzi hawa kutoka vyuo vya ufundi serikali imepenga kuanza kuwapatia mikopo ya masomo ili kupata idadi kubwa ya wanafunzi wanaojiunga na vyuo hivi na hapo itapatikana idadi kubwa ya bunifu itakayoendana na kasi ya mabadiliko yaliyopo kwa sasa katika sekta ya elimu.

Pia Prof.Mkenda amewataka NACTVET kufanya uchunguzi katika vyuo vyote vya ufundi ikiwa ni pamoja na VETA ili kuhakikisha vijana wanaoandaliwa wanakidhi katika soko la ajira ili kuhakikisha kuwa elimu wanayopewa inakwenda kuwasaidia.

"Niwatake mkafanye case study katika vyuo vyote vya ufundi ili kuhakikisha wanafunzi wote wanapatiwa elimu ambayo itakwenda kuwasaidia katika soko la ajira narudia tena kuwa mkafanye hivyo maana wazazi wanalipa pesa kwa ajili ya kuwasomesha watoto wao ili walete mafanikio katika nchi na familia kwa ujumla."Amesema Mkenda

Pia ameahidi kuwa serikali itafanya mpango wa maonyesho hayo kufanyika na upande wa Zanzibar ili kuendelea kudumisha Muungano. amewataka vijana wanaomaliza elimu ya kidato cha nne na kushindwa kuendelea na kidato cha tano kujiunga na vyuo vya kati na ufundi.

“Leo hii kuna vijana wengi wanamaliza kidato cha nne lakini sio wengi wanaoendelea na kidato cha tano na sita vlazima tuboreshe vyuo vyetu vya kati ili vijana ambao watashindwa kuendelea na maso

Waziri Jafo amesema serikali ya awamu ya sita imewekeza katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo itatanua wigo wa kuajiri vijana wenye umahili katika ufundi.

Alisema Tanzania inafanya uwekezaji mkubwa katika ujenzi wa bwawa la kufua umeme la mwalimu nyerere ambalo ujenzi wake unaendelea na utahitaji vijana ambao wana ujuzi wa kutosha.

Elimu ya ujuzi na sasa imeanza mchakato wa ku uendeshaji na ukarabati wa Kwa upande wake Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda amesema kuwa serikali ili kuendelea kukuza bunifu za wanafunzi hawa kutoka vyuo vya ufundi serikali imepenga kuanza kuwapatia mikopo ya masomo ili kupata idadi kubwa ya wanafunzi wanaojiunga na vyuo hivi na hapo itapatikana idadi kubwa ya bunifu itakayoendana na kasi ya mabadiliko yaliyopo kwa sasa katika sekta ya elimu.

Pia Prof.Mkenda amewataka NACTVET kufanya uchunguzi katika vyuo vyote vya ufundi ikiwa ni pamoja na VETA ili kuhakikisha vijana wanaoandaliwa wanakidhi katika soko la ajira ili kuhakikisha kuwa elimu wanayopewa inakwenda kuwasaidia.

"Niwatake mkafanye case study katika vyuo vyote vya ufundi ili kuhakikisha wanafunzi wote wanapatiwa elimu ambayo itakwenda kuwasaidia katika soko la ajira narudia tena kuwa mkafanye hivyo maana wazazi wanalipa pesa kwa ajili ya kuwasomesha watoto wao ili walete mafanikio katika nchi na familia kwa ujumla"Amesema Mkenda

Pia ameahidi kuwa serikali itafanya mpango wa maonyesho hayo kufanyika na upande wa Zanzibar ili kuendelea kudumisha Muungano.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad