HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 2, 2022

TMA yatoa ufafanuzi siku 90 za baridi, kipupwe, homa ya mapafu

 

Na Karama Kenyunko Michuzi TV
NDANI ya miezi mitatu kuanzia mwezi wa Juni hadi Agosti, Tanzania inatarajiwa kukutana na hali ya baridi, kipupwe ambacho kinaweza kusababisha baadhi ya maradhi kwa binadamu na wanyama katika kipindi hicho.

Mamlaka ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa ushauri na tahadhari kwa wadau wa sekta mbalimbali wanaotumia taarifa za hali ya hewa katika utekelezaji wa majukumu yao.

TMA imesema kwa kawaida, kipindi cha miezi ya Juni hadi Agosti, huwa ni kipindi cha baridi na upepo kwa maeneo mengi ya nchi, lakini kwa mwaka huu hali hiyo kuna uwezekano kuwa siyo kama ilivyokuwa katika miaka iliyopita.

Hali ya joto katika kipindi hicho cha miezi mitatu hali ya baridi na wastani hadi joto kiasi inatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi, lakini hata hivyo, hali ya joto kiasi hadi baridi ya wastani inatarajiwa katika maeneo ya ukanda wa pwani ya kaskazini pamoja na nyanda za juu kaskazini mashariki.

Mamlaka hiyo imeeleza kuwa katika kipindi hicho kutakuwa na vipindi vya upepo mkali vinatarajiwa kushamiri katika maeneo mengi nchini, ambao unatarajiwa utakaovuma kutoka kusini-mashariki na mashariki (Matlai).

Kutokana na hali hiyo kuna matarajio kutokea kwa baadhi ya athari za magonjwa ya mifugo yanayoambatana na baridi kama vile homa ya mapafu yanaweza kujitokeza lakini pia kunatarajiwa kuwa na vumbi inayoambatana na upepo mkali katika baadhi ya maeneo inatarajiwa kujitokeza na inaweza kuathiri afya ya binadamu na wanyama hasa mafua.

Hali hiyo ya joto kiasi, baridi na kipupwe inatarajiwa kuwa katika kiwango tofauti kulingana na maeneo ya kijografia ambapo katika kanda ya Ziwa Victoria yenye mikoa ya Mwanza, Mara, Geita, Kagera, Shinyanga na Simiyu, kiwango cha joto la chini kinatarajiwa kuwa cha kawaida hadi juu ya kawaida kati ya nyuzi joto 14 oC na 20 oC katika maeneo mengi.
Wakati ukanda wa pwani ya kaskazini inapopatikana mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga, maeneo ya kaskazini mwa mkoa wa Morogoro pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba, hali ya joto kiasi hadi baridi ya wastani inatarajiwa kuwa kati ya nyuzi joto 22 oC na 26 oC wakati maeneo ya mwambao wa pwani na visiwani na 18 oC na 22 oC na maeneno yenye miinuko hususan katika mikoa ya Tanga na Morogoro yanatarajiwa kuwa na kiwango cha nyuzi joto chini ya 18 oC.

Kanda ya nyanda za juu kaskazini mashariki katika mikoa ya mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara, hali ya joto kiasi hadi baridi ya wastani inatarajiwa katika maeneo mengi, kiwango hicho kinatarajiwa kuwa kati ya nyuzi joto 10 oC na 18 oC, lakini maeneno yenye miinuko yanatarajiwa kuwa na kiwango cha nyuzi joto chini ya 10 oC.

Katika kanda ya magharibi yenye mikoa ya Tabora, Rukwa, Katavi na Kigoma, hali ya baridi ya kawaida hadi joto kiasi inatarajiwa kuwa kati ya nyuzi joto 14 oC na 20 oC.

Kanda ya kati yenye mikoa ya Singida na Dodoma, hali ya baridi ya kawaida hadi joto kiasi inatarajiwa katika maeneo mengi ambapo joto linatarajiwa kuwa kati ya nyuzi joto 12 oC na 18 oC, wakati ukanda wa pwani ya kusini mikoa ya Mtwara na Lindihali ya baridi ya kawaida hadi joto kiasi inatarajiwa kuwa kati ya nyuzi joto 14 oC na 22 oC na mkoa wa Ruvuma unatarajiwa kuwa kati ya nyuzi joto 6 oC na 14 oC.

Hali ya hewa kayika ukanda ya nyanda za juu kusini-magharibi yenye mikoa ya Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe pamoja na maeneo ya kusini ya mkoa wa Morogoro, hali ya baridi ya kawaida hadi joto kiasi inatarajiwa kuwa kati ya nyuzi joto 4 oC na 14 oC, lakini katika maeneo ya miinuko kiwango hicho kinatarajiwa kuwa chini ya nyuzi joto 4 oC.

Dk. Ladislaus Chang’a, Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi ya Hali ya Hewa (TMA) ametoa tahadhari kwa upande wa wanyama kuwa wafugaji watumie kwa uangalifu matumizi ya maji na malisho kwani kunawekezana kutokea upungufu kutokana na hali hiyo itakayotokea katika kipindi hicho cha miezi mitatu.

Mkurugenzi huyo amesema pia amewataka wananchi kuchukua tahadhari za kiafya kwa kujikinga dhidi ya magonjwa yanayoweza kusababishwa na hali ya baridi, vumbi na matumizi ya maji yasiyo safi.

Wakulima nao hawakuachwa nyuma kwani wamehimizwa kulima mazao ya mbogamboga na mizizi kama vile viazi kwenye maeneo oevu ili kukabiliana na uhaba wa chakula utakaosababishwa na hali hiyo ya hewa.

TMA imeeleza kuwa licha ya hali ya ukavu ambayo inatarajiwa kuendelea katika kipindi hicho, upepo unaotarajiwa kuvuma kutoka kusini mashariki na mashariki unaweza kuleta unyevuunyevu kutoka Bahari ya Hindi na kusababisha vipindi vya mvua nyepesi katika maeneo machache ya Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na pwani ya kaskazini (mikoa ya Tanga, Dar es Salaam na Pwani).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad