HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 23, 2022

TIC YANUIA KUSIMAMIA UTATUZI WA CHANGAMOTO SEKTA YA UVUVI

Maftah Bunini, Mkurugenzi wa Utafiti, mifumo na mipango wa TIC akiwasilisha mada wakati wa mkutano na wadau wa sekta ya uvuvi jijini Mwanza.KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimefanya mkutano na wadau wa sekta ya uvuvi katika jitihada za kutambua changamoto mbalimbali za kisekta ili kuboresha mazingira ya Biashara na Uwekezaji nchini. Mkutano huo umefanyika jijini Mwanza Hotel ya Gold Crest katika ukumbi wa Bismarck leo tarehe 22 June, 2022.

Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ndugu Joachim Otaru akifungua mkutano huo amesema asilimia 53 ya Mkoa wa Mwanza ni maji na asilimia 47 ni ardhi na sehemu kubwa ya ziwa Victoria haijatumika ipasavyo. Kuna fursa nyingi katika ziwa ikwamo ufugaji wa samaki, utalii ndani ya maji na ujenzi wa viwanda katika kuongeza minyororo ya thamani katika maji kwa ajili ya uchumi wa bluu.

Akizungmza katika mkutano huo bwana Maftah Bunini ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa TIC amesema sekta ndogo ya uvuvi ni nuhimu sana katika maendeleo ya nchi yetu na mpaka sasa uwekezaji kwenye sekta hiyo umeleta ajira zaidi ya milioni nne (4) na kuchangia takribani asilimia 1.4% ya pato la Taifa. Mjadala huu ni muhimu ili kutambua changamoto, kujadili njia bora za kutatua changamoto hizo na mapendekezo yatakayochukuliwa kupelekwa serikalini kwa ajili ya kujadiliwa na kupata suluhisho za changamoto hizo aliongeza Bw. Bunini.

Bw. Bunini amesema TIC imesajili miradi 165 ya sekta ndogo ya uvuvi yenye thamani ya zaidi ya dola za kimarekani milioni 588.63 na inatarajia kuzalisha ajira zaidi ya 25,269 na hii inaonyesha umuhimu wa sekta hii katika kusaidia maendeleo ya uchumi wa nchi yetu.

Naye Onesmo Sulle Katibu wa chama cha wenye viwanda vya kuchakata na kusindika samaki TIFPA ameishukuru serikali kwa kufikiria kupunguza mrahaba wa kutoka senti 20 za dola ya Marekani kwenda senti 10 lakini ameomba serikali iendelee kufikiria kupunguza kwa maana ukilinganisha na nchi jirani ya Uganda na Kenya Tanzania bado malipo ya mrahaba bado ni makubwa hata baada ya pendekezo la kupunguzwa.

Naye Mecky Sadick ameomba serikali itoa msamaha wa kodi kwenye mabomba ya HDP ili kwa ajiki ya kutengeza vizimba ili kuweza kuhamasisha uwekezaji katika ujenzi wa vizimba imara katika ufugaji wa samaki kwenye vizimba kwani ni chachu ya uvuvi endelevu.
Wadau walioshiriki kikao hicho ni wamiliki wa Viwanda vya kuchakata Samaki, Taasisi za Serikali NEMC, BRELA, TRA, TAFIRI na Idara ya Uvuvi, Wavuvi, Wafugaji wa Samaki kwa njia ya Vizimba (Fish caging and agriculture), Uongozi wa Mkoa wa Mwanza na Taasisi za fedha NMB, TIB, TPB na CRDB.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad