HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 10, 2022

TASAC: Biashara ya Meli inalipa


Kaimu Meneja Masoko na Uhusiano, Shirika la Uwakala wa Meli  Tanzania (TASAC), Josephine Bujiku akizungumza na  Wahariri, Waandaaji wa Vipindi na waandishi wa habari wakati wa Mafunzo yaliyotolewa kwa Siku mbili na Shirika la Uwakala wa Meli  Tanzania (TASAC) Bagamoyo Mkoani Pwani Juni 9, 2022.

*Serikali iliona mbali kuanzisha TASAC

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania  (TASAC), imesema biashara ya bandari inalipa na inafanya uchumi wa nchi kupaa kutokana na kuhudumia meli kwa wakati.

Serikali imejipanga kuja na mkakati mkubwa  wa kuongeza miundombinu ya bandari kurahisisha upakuaji wa shehena mbalimbali na kupunguza mzigo mkubwa uliopo katika Bandari ya Dar es Salaam kwa sasa kwani wakati mwingine meli nyingi zinazoingia na hivyo kusababisha meli nyingine kushindwa kutia nanga kutokana na kukosa nafasi. 

Kwa mujibu wa TASAC, hivi karibuni, washirika hao wanaofanya kazi za kuhudumia biashara zinazotumia bandari, walifanya vikao vya kujipanga ili kufanya maboresho katika bandari nyingine ili kuifanya ile ya Dar és Salaam ipumue kutokana na idadi kubwa ya meli zinazotia nanga.

Hayo yamebainishwa na  Afisa Mwandamizi wa Uwakala wa Meli wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania  (TASAC), Gabriel Anthony wakati akiwasilisha mada katika semina ya Wahariri, waandaaji wa Vipindi na waandishi wa Habari iliyoandaliwa na TASAC Bagamoyo mkoani Pwani.

"Bandari ya Dar es Salaam  inahitaji kupumua katika kuipunguzia mzigo kuna haja ya kuboresha bandari zetu nyingine. Kwa mfano wateja wanaotoka katika mikoa ya Arusha au Kilimanjaro watumie Bandari ya Tanga kupokea mizigo yao." Alisema Anthony.

"Au wale waliopo katika mikoa ya Ruvuma na mikoa ya karibu mizigo yao wawe wanapokea katika bandari ya Mtwara, ikifanyika hivo itasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza mzigo mkubwa uliopo katika bandari ya Dar és Salaam."

Anthony amesema mbali na kuboresha bandari zilizopo pia kunatakiwa kujengwa magati mapya ili kuhakikisha biashara hiyo ya usafirishaji majini inafanyika kwa ufanisi.

"Bandari kavu nazo zinasaidia kupunguza mzigo uliopo katika bandari ya Dar és Salaam, lakini hii bado haitoshi, ndio maana tunasema bado kunahitajika maboresho zaidi katika bandari nyinginezo, "alisema. 

Pia, amesema bado kuna changamoto ya uwezo wa uwezo wa bandari katika kuhudumia ongezeko la meli zinazoingia nchini kupitia bandari hizo.

Kwa mfano wakati mwingine meli zimekuwa zikitumia muda mwingi kusubiri kuingia kwenye gati, hali hii inaathiri mzunguko wa safari na soko la bandari,"alisema. 

Anthony amesema biashara ya Uwakala wa Meli ikisimamiwa vizuri na kufanywa kwa uadilifu, umakini na weledi ni miongoni mwa biashara bora yenye mchango mkubwa kwa uchumi wa nchi.

Anthony amesema katika kufanikisha biashara hiyo ya Uwakala wa Meli, kuna haja kwa wasimamizi wa biashara hiyo nchini kusimamia vizuri na kuifanya kwa uadilifu wa hali ya juu, umakini na weledi kwa masilahi ya nchi.
Mhariri wa Gazeti la Uhuru Mariam Mziwanda akizungumza na  Wahariri, Waandaaji wa Vipindi na waandishi wa habari wakati wa Mafunzo yaliyotolewa kwa Siku mbili na Shirika la Uwakala wa Meli  Tanzania (TASAC) Bagamoyo Mkoani Pwani Juni 9, 2022.
 Mkurugenzi wa Fedha na Uhasibu Shirika la Uwakala wa Meli  Tanzania (TASAC), CPA Habibu Saulo akizungumza na  Wahariri, Waandaaji wa Vipindi na waandishi wa habari wakati wa Mafunzo yaliyotolewa kwa Siku mbili na Shirika la Uwakala wa Meli  Tanzania (TASAC) Bagamoyo Mkoani Pwani Juni 9, 2022.
Afisa Mwandamizi, tozo na Ushindani, Shirika la Uwakala wa Meli  Tanzania (TASAC), Chester Kapinga akizungumza na  Wahariri, Waandaaji wa Vipindi na waandishi wa habari wakati wa Mafunzo yaliyotolewa kwa Siku mbili na Shirika la Uwakala wa Meli  Tanzania (TASAC) Bagamoyo Mkoani Pwani Juni 9, 2022.
Afisa Mwandamizi- Wakala wa Meli, Shirika la Uwakala wa Meli  Tanzania (TASAC), Gabriel Anthony akizungumza na  Wahariri, Waandaaji wa Vipindi na waandishi wa habari wakati wa Mafunzo yaliyotolewa kwa Siku mbili na Shirika la Uwakala wa Meli  Tanzania (TASAC) Bagamoyo Mkoani Pwani Juni 9, 2022.
 Karani Mwandamizi- Uhakiki shehena Shirika la Uwakala wa Meli  Tanzania (TASAC), Jenifa Matemba akizungumza na  Wahariri, Waandaaji wa Vipindi na waandishi wa habari Mafunzo aliyotolewa kwa Siku mbili na Shirika la Uwakala wa Meli  Tanzania (TASAC) Bagamoyo Mkoani Pwani Juni 9, 2022.

Afisa Mkuu wakala wa Forodha Shirika la Uwakala wa Meli  Tanzania (TASAC), CPA Michael Polycarp akizungumza na  Wahariri, Waandaaji wa Vipindi na waandishi wa habari Mafunzo aliyotolewa kwa Siku mbili na Shirika la Uwakala wa Meli  Tanzania (TASAC) Bagamoyo Mkoani Pwani Juni 9, 2022.



 Baadhi ya Wahariri, Waandaaji wa Vipindi na waandishi wa habari wakiwa katika  Mafunzo yaliyotolewa kwa Siku mbili na Shirika la Uwakala wa Meli  Tanzania (TASAC) Bagamoyo Mkoani Pwani Juni 9, 2022.
Kutoka kulia ni Karani Mwandamizi- Uhakiki shehena Shirika la Uwakala wa Meli  Tanzania (TASAC), Jenifa Matemba, Afisa Mwandamizi- Wakala wa Meli, Shirika la Uwakala wa Meli  Tanzania (TASAC), Gabriel Anthony, Afisa Mkuu wakala wa Forodha Shirika la Uwakala wa Meli  Tanzania (TASAC), CPA Michael Polycarp na  Afisa Mwandamizi, tozo na Ushindani, Shirika la Uwakala wa Meli  Tanzania (TASAC), Chester Kapinga wakiwa katika picha ya pamoja.

Picha za pamoja kati ya wafanyakazi wa Shirika la Uwakala wa Meli  Tanzania (TASAC), Chester Kapinga na  Wahariri, Waandaaji wa Vipindi na waandishi wa habari wakiwa katika  Mafunzo yaliyotolewa kwa Siku mbili na Shirika la Uwakala wa Meli  Tanzania (TASAC) Bagamoyo Mkoani Pwani Juni 9, 2022.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad